The House of Favourite Newspapers

GLOBAL TV: Chaneli namba 1 mtandaoni Kuwa na taarifa ya habari

SI jambo dogo hata kidogo! Ilianza kwa kurusha ‘live’ matukio mbalimbali na kuwa chaneli namba moja ya mtandaoni (online) kurusha live matukio yote yanayotikisa Tanzania kisha wengine wakafuata baadaye.

Good news nyingine ni kwamba Global TV ndiyo chaneli namba moja kwa kurusha taarifa ya habari na hadi sasa hakuna chaneli inayoisogelea.

TUJIUNGE NA MAKAO MAKUU

Akizungumza na Ijumaa, Mkuu wa Idara ya Global TV yenye makao yake makuu kwenye Jengo la Global Group lililopo Sinza-Mori jijini Dar, James Range anasema kwamba Global TV tangu imeanza imeweza kuwa na vitu vya kipekee ambavyo huwezi kuvipata kwenye chaneli ya aina yoyote ya mtandaoni.

“Tumekuwa wabunifu kila siku, kama mtakumbuka tulianza na kurusha matukio yote yanayotokea ambayo ni gumzo, sisi tulikuwa wa kwanza kuyarusha live kutoka eneo la tukio, baada ya muda kidogo, wengine wakafuata.

“Sasa tuna taarifa ya habari inayotambulika kama Global Habari, hii nayo ni ya kipekee kwani hakuna chaneli ya online inayorusha taarifa ya habari,” anasema Range.

IPOJE?

Akifafanua juu ya hilo, Range anasema kuwa, taarifa ya habari huruka kila siku kuanzia saa 12:30 jioni ikiwa imejaa taarifa zote kuanzia za kitaifa, kimataifa, biashara na michezo.

“Tuna watangazaji mahiri wa taarifa ya habari ambao ni Catherine Kahabi na Felister Massae. Pia katika kipengele cha habari za kimataifa huwa tunajiunga moja kwa moja na Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika (VOA) ambapo hukuletea habari zote za kimataifa zilizotokea kwa siku husika.

“Kabla taarifa ya habari haijaisha, huwa tuna uchambuzi maalum ambao hukuchambulia yale yote yaliyotokea kwa siku husika chini ya wachambuzi mahiri wa habari za kina, Aziz Hashim, Sifael Paul na Elvan Stambuli,” anasema Range.

Range anaendelea kuwa, kila siku ifikapo saa 2:00 usiku, Global TV hujiunga moja kwa moja na TBC1 na kukuletea taarifa ya habari nyingine hivyo kutoa nafasi kubwa hata kwa wale ambao wako mbali na TV.

VINGINE HIVI HAPA

Range anasema kuwa, Global TV imedhamiria kukata kiu ya watazamaji wa vipindi tofauti vya online ambapo mbali na Global Habari, kila siku saa 12:30 asubuhi kuna Kipindi cha Amka na Global TV.

“Amka na Global TV ni kipindi cha uchambuzi wa magazeti yote ya siku husika kinachoongozwa na mtangazaji Aron Felix. Hili nalo hakuna chaneli yoyote ya online inayofanya hivi zaidi ya Global TV.”

MICHEZO TUPO

Range anaongeza kuwa, kuna kipindi namba moja cha michezo online kiitwacho Spoti Hausi kinachojiri kila siku ya Alhamisi kuanzia saa 10:00 jioni kikiongozwa na watangazaji mahiri, Wilbert Moland, Phillip Nkini na Saleh Ally ‘Jembe’.

BURUDANI IPO

“Kwa wale wapenda burudani, tuna Kipindi cha Global Entertainment ambacho hukuangazia yale yote yanayojiri kwa upande wa burudani ndani na nje ya Bongo. Hapa kuna utofauti mkubwa wa chaneli pengine hata TV yoyote kwani Global TV huwa ya kwanza kukuhabarisha yote yanayotokea katika tasnia ya burudani kwa siku husika. Kipindi hiki huruka hewani kila siku ya Jumamosi saa 5:00 asubuhi kikiongozwa na watangazaji wakali akiwemo Given Mashishanga,” anasema Range.

HADI WAPENDA FILAMU

Range anaendelea kusema kuwa, mbali na vipindi hivyo kuwa rasmi kila siku husika, Global TV ‘imekava’ kila sekta kuanzia kijamii, kisiasa hadi kiburudani.

“Wale wapenda tamthiliya kuna Kipindi cha Short Films kinachoonesha filamu fupifupi. Pia tuna Global Kazini kirukacho kila mwanzo wa mwezi kikionesha matukio ya kukushangaza yanayojiri ndani ya Ofisi za Global Publishers zilizopo Sinza-Mori jijini Dar.

“Wale wapenda urembo tuna Kipindi cha Beauty & Styles kinachoongozwa na Catherine Kahabi, Minyoosho ambacho kinadili na wale mastaa wanaofeki maisha kinachoongozwa na mtangazaji mahiri, Flora Mvungi na Old is Gold cha watu mashuhuri waliotikisa zamani,” anamaliza Range.

VOA NDANI

Wale wapenda kujua yanayojiri nje ya nchi, Global TV kwa kushirikiana na VOA wamekuletea vipindi baab’kubwa kama vile Shaka Ssali Extra Time kinachoruka kila siku ya Jumatano saa 5:00 asubuhi na Straight Talk Africa kila Alhamisi saa 5:00 asubuhi.

“Kila siku ya Jumanne saa 5:00 asubuhi tuna Kipindi cha Washington Bureau kinachoongozwa na mtangazaji mkongwe na mahiri, Sunday Shomari,” anasema Range.

UNAIPATAJE HIYO GLOBAL TV?

Ni rahisi sana, ili uwe unapata habari papo hapo kuanzia kwenye simu yako, tableti, laptop au kompyuta yako, ingia kwenye Mtandao wa Youtube kisha andika Global TV Online baada ya kuingia, jisajili (subscribe) bila kusahau kubonyeza kengele pembeni yako ili uwe unajulishwa kinachoendelea.

APP PIA IPO

Global TV pia inapatikana kupitia Application ‘App’. Unachotakiwa kufanya ni kuwa na simu yako au tableti kisha ingia kwenye Play Store kwa wale watumiaji wa Adroid na utafute Global Publishers (utaona neno GP la rangi nyekundu) baada ya hapo install kisha utaweza kuona kila kitu humo ndani kuanzia Global TV, Magazeti ya Global Publishers na vingine vingi

Makala: Andrew Carlos, Dar

 

Bofya ==> Global TV Online

Comments are closed.