The House of Favourite Newspapers

GLOBAL TV YAPATA SHAVU MKUTANO WA KIMATAIFA

Mkuu wa Global TV Online, James Range akiwaeleza Mameneja wa Vituo vya Televisheni, Afrika Mashariki na Kusini waliohudhuria mkutano huo namna Global TV Online inavyofanya kazi.

GLOBAL TV ONLINE ambayo ni televisheni namba moja ya mtandao nchini Tanzania, imepata shavu baada kualikwa kushiriki katika semina ya Wakuu wa Vituo zaidi ya 28 vya Televisheni kutoka nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika.

 

Katika semina hiyo iliofadhiliwa na Sauti ya America VOA na BBG Direct, inafanyika kwa siku nne jijini Nairobi Nchini Kenya kuanzia Agosti 11 hadi kesho Agosti 14, 2018 ikiwa na lengo la kuwafundisha viongozi hao namna ya kuandaa vipindi bora vya televisheni na kuviendesha kwa mafanikio makubwa.

 

Globala TV Online ambayo imewakilishwa na kiongozi wake, James Range ndiyo televisheni pekee ya mtandaoni iliyoteuliwa kushiriki mafunzo hayo kutokana kufuatiliwa na watu wengi nzaidi mtandaoni na ubora wa kazi inazofanya ya kuuhabarisha na kuuelimisha umma.

 

Mbali na Tanzania, nchi nyingine zinzashiriki kutoka Afrika Mashariki ni Kenya, Uganda na Rwanda huku ukanda wa Afrika Kusini ukiwakilishwa na Zambia, Botswana, Zimbabwe, Afrika Kusini, Eswatin zamani Swaziland, Lesotho, Zanzibar na Malawi.

Subscribe Bofya ==> Global TV Online

Comments are closed.