Global wagawa ving’amuzi vya Ting kwa washindi
Mhariri wa Gazeti la Uwazi, Elvan Stambul (Kulia) akigawa zawadi ya King’amuzi cha Ting kwa mshindi, Fadhil Abdallah Chaurembo wa Magomeni jijini Dar.
Mhariri wa magazeti ya Global, Erick Evarist (kushoto) akigawa zawadi ya King’amuzi cha Ting kwa Jackson Maligo niaba ya mshindi, Gasper V. Massawe.
Washindi wa Chemsha Bongo na Ving’amuzi vya Ting inayoendeshwa na Magazeti ya Global Publishers (Uwazi na Amani) wamepatikana leo.
Chemsha Bongo hiyo inapatikana katika magazeti (Amani na Uwazi) ambapo msomaji unatakiwa kununua kisha kujibu maswali yaliyomo kwenye magazeti hayo na kupata nafasi ya kujishindia king’amuzi.