Global Watoa Mabati 500 Kwa Waathirika wa Tetemeko, Kagera
Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, Eric Shigongo (kushoto) akimkabidhi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Majaliwa Kassim Majaliwa msaada wa mabati mia tano kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi lilitokea hivi karibuni mkoani Kagera.
…Makabidhiano yakiendelea.
Eric Shigongo akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) baada ya kukabidhi mabati hayo.
… Eric Shigongo akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa Global Publishers kabla ya kukabidhi mabati hayo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, Eric Shigongo, leo amemkabidhi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Majaliwa Kassim Majaliwa msaada wa mabati mia tano kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la aridhi lilitokea hivi karibuni mkoani Kagera.
Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika ofisini kwa waziri mkuu jijini Dar es Salaam ambapo pia wawakilisha wa makampuni pamoja na taasisi mbalimbali walijitokeza pia kutoa michango yao kwa ajili ya kuwasaidia waathirika hao.
Comments are closed.