The House of Favourite Newspapers

#GlobalCelebrityUpdates: Kumbe Hii Ndio Sababu Kubwa Iliyompelekea Patoranking Kufanya Muziki Wa Raggae Dancehall.

Patoranking ni miongoni mwa wasanii wakubwa na wanaoheshimika kwenye soko la muziki la Africa kutokana na uimbaji wake wa miondoko ya Raggae Dancehall. Wengi wetu tunausikiliza na kuupenda muziki wake lakini hatufahamu kwanini Patoranking aliamua kuimba aina hiyo ya muziki.

Nimekutana na stori iliyonifurahisha kidogo kuhusiana na staa wa muziki kutoka Nigeria, Patoranking.

Inawezekana unafahamu au hufahamu lakini amini usiamini Patoranking hakupanga kuimba aina ya muziki anaouimba sasa na wala hakufikiria kuwa muziki Raggae Dancehall ndio ungemtoa kimaisha na kumtambulisha kwenye soko la muziki Africa na duniani kwa ujumla, ila maamuzi hayo yalitokana na kuamini kuwa kuimba muziki huo ungemuweka karibu na watoto wa kike:

Moja ya sababu zilizonifanya nichague raggae hata kama mtanicheka ni kwasababu wa wasichana. Nakumbuka kipindi hicho nipo sekondari, kama ulikuwa hujui jinsi ya kuimba nyimbo za raggae, ulikuwa huwezi kupata watoto wazuri na mimi ni mtu ambaye napenda kuonekana.

Kwahiyo nikaona itakuwa poa kuimba flow za nyimbo ambazo wenzangu hawazijui, nikawa nasikiliza sana nyimbo za raggae, na kila nilivyojitokeza kuimba aina hizo za nyimbo wasichana wengi walivutiwa na mimi, nikaona hili ni dili! Nikaanza kusikiliza nyimbo nyingi za Bob Marley na Lucky Dube kuanzia hapo…” – Patoranking.

Patoranking alisikia akisema kwenye moja ya interviews alizofanya weekend iliyopita.

Imeandikwa na: Sandra Brown.

Subscribe kwenye YouTube Chanel yetu ya Global TV Online ili zote kali zinazotufikia iwe ni siasia, michezo, comedy, burudani, muziki na mengineyo yakufikie  kwa wakati.

Comments are closed.