The House of Favourite Newspapers

#GlobalUpdates: Bongo Movie Bado Ina Uwezo Wa Kwenda Kimataifa Kwasababu Hii… (+Video)

Najua nina wadau wangu wengi kutoka Tanzania na nchi jirani za East Africa ambao ni wafuatiliaji na wapenzi wa kubwa wa Filamu zetu za Bongo Movie, na penigne huumizwa pale wanapoona tasnia hiyo ikirudi nyuma badala ya kwenda mbele… Usife moyo maana Mtanzania Ernest Napoleon anatuambia bado tunayo chance ya kufanya makubwa!

Kama umeshawahi kutizama movie ya ‘Going Bongo’ basi jina la Ernest Napoleon sio geni kwako. Mtanzania huyo kwa sasa yupo tayari kuileta kwetu filamu yake ya pili iitwayo ‘Karibu Kiumeni’, na jana  Ernest alifanya media screening exclusive kwa ajili ya Media na kuiongelea filamu hiyo mpya:

Moja ya vitu tulivyotaka kufanya kwenye hii filamu ni pamoja na kuiinua Industry ndio maana unaona tumeaalika watu wa Press waingalie movie kwanza kwasababu watu wa media ni watu muhimu na influencial wanaoweza kuiambia public kama movie hii ni ya kuiangalia au ni movie ya kuikosa“.

Ernest aliendelea kusema kuwa filamu za Bongo Movie bado zina nafasi kubwa ya kushindana kwenye soko la kimataifa kwakuwa lugha yetu ya Kiswahili kwa sasa ni miongoni mwa lugha zinazofuatiliwa sana duniani:

Lugha yetu ya Kishwahili inaongelewa na watu karibia Million 200, Filamu hazina sababu za kutokupata rankings kubwa na kwenda kimataifa, kwenda Rwanda, kwenda Kenya na kwengine. Kwasababu watu Milioni 200 ni idadi kubwa ya watu ambayo inaturuhusu sisi kuwa na Industry kubwa tu ya Filamu ambayo inaweza kuja kushindana na Industry nyingne kama Nollywood na Bollywood…” – Alisema Ernest.

Mtazame Ernest Napoleon akiiongelea filamu yake mpya ‘Karibu Kiumeni’ kwenye hizi dakika tano hapa chini.

Karibu Kiumeni ni filamu ya pili ya Ernest Napoleon na itaanza kuonyeshwa kwenye kumbi za Sinema za Mlimani City kuanzia tarehe 17 Machi kwa muda wa wiki mbili. Ndani ya filamu hiyo tutaweza kuona baadhi ya wakali wa Bongo Movie kama Muhogo Mchungu na Irene Paul huku sura ama vipaji vipya vitakavyoonekana ni pamoja na Idris Sultan na Miss (Antu) Mandoza.

Itazame trela ya Karibu Kiumeni hapa chini:

 

Imeandikwa Na: Sandra Brown

Subscribe kwenye YouTube Chanel yetu ya Global TV Online ili zote kali zinazotufikia iwe ni siasa, michezo, comedy, burudani, stori za mastaamuziki na nyingine zikufikie kwa wakati.

 

Comments are closed.