#GlobalUpdates: Kampuni Ya Nike Kuja Na Hijab Za Mazoezi Kwa Ajili Ya Dada Zetu Wa Kiislam – (Pichaz/Video)

Mazoezi ni kitu muhimu sana kwa mawanadamu na ndio maana Nike hawataki kumuacha mtu nyuma.

Kama wewe ni mpenda mazoezi na hutamnai sana kufanya mazoezi yako kwa uhuru bila kuhisi umevaa nguo zinazokuchorehsa mwili sana basi ondoa shaka Nike inakuja na kitu sahihi kwa ajili yako.

Nimetembelea mtandao wa Al Arabiya Network na kuipata hii ya kampuni maarufu ya nguo za michezo, viatu pamoja na vifaa vyake Nike kujipanga kuwabeba dada zetu wa kiislam wenye mapenzi ya kujiweka fit lakini hushindwa kufanya hivyo kwa kukosa nguo sahihi.

Kwa mujibu wa press statement iliyotolewa na msemaji mkuu wa kampuni ya Nike Megan Saalfeld kwenye mtandao wa Al Arabiya Networknia na dhumuni la kutengeneza vazi hili ni kuwapa urahsi wanawake wa kiislam kushiriki kwenye michuano mbalimbali kwa uhuru zaidi:

Hijab hii ya Nike Pro – Hijab ni wazo lililotokana na kuona wadada wengi wa kiislam wanakosa vazi lao maalum la kuvaa kwenye mazoezi na mashindano mengine ya michezo hivyo kulazimika kuvaa hijab pamoja na tracksuits ili kuweza kishiriki kwenye michuano mbalimbali ya michezo.

Tumekuwa tukiendelea kuliboresha vazi hili kwa takriban mwaka sasa kwasababu nia yetu ni kutengeneza vazi litakalokuwa jepesi mwilini, lisilokusanya joto jingi, na vazi lenye uwezo wa kuvaliwa na kuvuliwa kiurahisi bila kuchukua muda mwingi. ” – Megan Saalfeld.

Sababu nyingine iliyotusukuma kutengenza vazi hili ni kutokana na muamko mkubwa wa wanawake wa kiislam kushiriki kwenye mashindano na michuano mbalimbali ya michezo, ni muamko unaokua kwa kasi kubwa sana kwa wanawake wa imani hiyo baada ya mwanariadha moja kutoka nchi za kiarabu kuchukua medali ya ushindi mwaka 2012 jijini London.

Tunategemea hijab hizi zitawasaidia wanawake hawa kuwa na uhuru mkubwa zaidi wa kufanya mazoezi na kufanya vizuri zaidi kwenye mashindano mbalimbali. ” – Megan Saalfeld.

Hijab hizo zinategemea kuingia sokoni mwaka 2018 na zitakuwa zinapatikana kwenye rangi tatu, nyeusi, kijivu na obsidian.

Hapa chini ni picha zote nne za jinsi vazi hilo litakavyokuwa na kuvaliwa:

Kaa Karibu na sisi kwa updates zaidi juu ya hii taarifa.

 

IMEANDIKWA NA: Sandra Brown.

Subscribe kwenye YouTube Chanel yetu ya Global TV Online ili zote kali zinazotufikia iwe ni siasa, michezo, comedy, burudani, stori za mastaa, updates mbalimbali, muziki na nyingine zikufikie kwa wakati.
Toa comment