The House of Favourite Newspapers
gunners X

Godbless Lema Apewa Hifadhi Canada

0

ALIYEKUWA mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Godbless Lema, amepata  hifadhi ya kisiasa nchini Canada.

 

Lema aliondoka jana nchini Kenya akiwa na familia yake kuelekea nchini Canada ambapo wakili wake, George Luchiri Wajackoyah, amethibitisha.

 

Mwezi uliopita Lema, alikamatwa na Jeshi la Polisi nchini Kenya kwa madai ya kuingia nchini humo kinyume na sheria na kumuachia huru baada ya muda mfupi.

 

Kwa mujibu wa wakili wake huyo, Lema ambaye ameambatana na familia yake alikuwa akielekea jijini Nairobi kwa ajili ya kutafuta makazi ya muda baada ya kudai kutishiwa maisha.

Leave A Reply