Gold Edition Party ya Johnnie Walker Gold Label Yawasha Moto Tips Coco Beach
Jumamosi iliyopita, tulikuwa kwenye machimbo ya pale Tips Coco Beach katika tukio la Squishy Life. Burudani ilikuwa ya kibabe ikisindikizwa na upepo mwanana wa bahari, mataa ya jiji na dhahabu dhahabu kila mahali!
Chupa ya Johnnie Walker Gold Label ilikuwa ya kuvutia sana ikisindikizwa na msafara wa warembo wasiopungua nane waliovalia rangi za dhahabu, wenye maji na makubwa na cheche za taa kuitambulisha “Golden Chalice”.
Ukumbi mzima ulijaa watu maarufu kutoka Dar; Pongezi nyingi kwa Luge, Uncles, Dar People, Elcasa, Str8 Up Vibez na DJs wote. Tuliwaona! #LivingGolden.
Mzuka wa usiku huo ulikuwa na mchanganyiko wa radha mbalimbali za muziki ambazo ziliongeza mzuka! Kuanzia midundo laini ya R&B mpaka Amapiano iliyopigwa na DJ mgeni kutoka Afrika Kusini, Kmat. Wimbo wa MKK X Cow Boi ulikuwa mkali sana!
Mchanganyiko wa muziki mzito, muonekano mzuri, na kinywaji cha dhahabu cha viwango vya juu kilichofanya usiku huo kuwa wa kipekee na wenye burudani ya kusisimua.
Sherehe ya Gold Edition haikuwa tu tukio—ilionesha ubora wa kipekee wa kinywaji bomba cha Johnnie Walker Gold Label, jioni moja ambayo watu mashuhuri wa jiji la Dar walikusanyika kusherehekea kwa viwango na burudani ya kutosha.
Kaa tayari kwa ajili ya kifuatacho! Self-plug @johnniewalker_tz
#KeepWalking