Kartra

Gomes Aifanyia Umafia Yanga

KUELEKEA mchezo wao wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga utakaopigwa Septemba 25, mwaka huu, Benchi la Ufundi la Simba chini ya Kocha Mkuu, Didier Gomes, limepanga kufanya umafia kuwasoma wapinzani wao hao.

 

Simba wamesema kwamba, kabla ya kukutana na Yanga, wataichunguza timu hiyo namna ya inavyocheza sambamba na ubora wa kikosi chao kwenye mechi zao mbili za Ligi ya Mabingwa Afrika itakapocheza dhidi ya Rivers United ya Nigeria.

Chanzo chetu kutoka ndani ya Simba, kimeliambia Spoti Xtra kuwa: “Tumewaona Yanga katika mchezo uliopita dhidi ya Zanaco, lakini kwa kuwa mchezo ule haukuwa wa kimashindano, sasa benchi la ufundi chini ya Kocha Gomes linajiandaa kuwachunguza zaidi wapinzani wetu hao katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, ili kujua ubora na mapungufu waliyonayo kwa ajili ya kuhakikisha tunawafunga.”


Toa comment