The House of Favourite Newspapers

Gomes Aingilia Dili la Zimbwe Kutua Yanga

0

KOCHA Mkuu wa Simba, Mfaransa Didier Gomes amegoma kuona mastaa wake wakiondoka kwenye kikosi chake katika msimu ujao.

 

Kati ya mastaa wanaotajwa kuondoka Simba ni Mohammed Hussein ‘Zimbwe Jr’ anayedaiwa kusaini mkataba wa awali Yanga, Joash Onyango kwenda Orlando Pirates na Aishi Manula kuwaniwa na Mamelodi Sundowns zote za Afrika Kusini.

 

Zimbe Jr au Tshabalala na Manula hivi sasa wanaelekea kuwa wachezaji huru kwa kuwa mikataba yao inaelekea mwishoni.

 

“Muda wa usajili bado lakini nimeona vema kulizungumzia hili la wachezaji wangu wanaodaiwa kuondoka Simba mwishoni mwa msimu huu baada ya mikataba yao kumalizika.“

 

Binafsi sitakubali kuona wachezaji wangu hao wakiondoka kutokana na umuhimu mkubwa waliokuwa nao katika timu, kwani siku zote ni hatari kwa timu kufanya mabadiliko ya kikosi kwa kuwaondoa wachezaji walioipa mafanikio timu hasa msimu huu kimataifa.

 

“Lakini kingine sifahamu kuhusu kuondoka kwao, kitu kikubwa nitakachoweza kusema kuwa natamani kubakia na wote katika misimu mingine miwili hadi mitatu katika kutengeneza timu bora kwa ajili ya mafanikio ya timu,” alisema Gomes.

STORI: WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam

Leave A Reply