The House of Favourite Newspapers

Gomes Ana Hasira na Yanga

0

HASIRA za Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes kwa sasa zipo katika kubeba makombe mawili ya ndani ambayo anashindania sambamba na watani zao wa jadi, Yanga.

 

Gomes amepania kumaliza msimu huu kwa kutetea mataji yao waliyoyatwaa msimu uliopita ambayo ni Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho la Azam.

 

Tayari ndani ya Ligi Kuu Bara, Simba ndiyo vinara wakiwa na pointi 61 baada ya kucheza mechi 25, huku wakiwa robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo wanakwenda kucheza dhidi ya Dodoma Jiji, Jumatano ijayo.

Akizungumzia mikakati yao, Gomes alisema: “Kikubwa ni kuangalia namna ya kutetea mataji yetu msimu huu, haitakuwa rahisi kwetu kuona tunayapoteza na kwenda sehemu nyingine.

 

Tutapambana kwa nguvu zote kutetea.”Msimu huu ikitokea Simba ikabeba tena mataji hayo, itakuwa ni msimu wa nne mfululizo Yanga inakosa ubingwa wa Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho la Azam.

Leave A Reply