The House of Favourite Newspapers

Gomes Awashushia JKT Muziki Mnene

0

KUWACHAPA wababe wa Afrika, Waarabu Al Ahly kwa bao 1-0 kumewazidisha jeuri mashabiki wa Simba ambao kwa sasa wametamba kwamba hata wawapangie kikosi gani wapinzani wao Yanga basi wanaamini wataacha pointi tatu wakikutana nao.

 

 

Simba hivi sasa huwaambii kitu kuhusiana na kikosi chao ambacho ndicho pekee kilichoweza kushinda mechi mbili za kwanza za hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Yaani hakuna timu nyingine yoyote kwenye ligi hiyo ambayo imefanikiwa kufanya hivyo.

 

 

Jeuri hiyo ya Simba kuwatambia watani wao Yanga, inakuja kutokana na ukubwa wa kikosi chao, aina ya wachezaji na aina ya matokeo ambayo wamekuwa wakiyapata kwenye mechi za Ligi Kuu Bara, Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC), maarufu kama Kombe la FA na zile za Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

 

Kikosi hicho cha Simba ambacho kinafundishwa na Mfaransa, Didier Gomes, kinaundwa na wachezaji 30 ambao wamegawanywa kwenye makundi mawili, wale ambao wanacheza ligi na michuano ya kimataifa na wengine wakiwa kitaifa pekee.

 

 

Kama utaamua kuwagawa wachezaji hao 30 wa Simba, unapata vikosi vitatu ambavyo unaweza kuvitumia kucheza katika mechi yoyote ikiwemo na Yanga ambao kwa siku za karibuni wamekuwa na mwendo usio wa kuridhisha, na ukapata matokeo mazuri.

 

 

Kikosi cha kwanza kati ya wachezaji hao 30 ni kile ambacho kimekuwa kikitumiwa mara kwa mara na Gomes kwenye mechi hasa za kimataifa na kilichoshinda mbele ya Al Ahly na AS Vita ambacho kitaundwa hivi; kipa Aishi Manula huku mabeki wakiwa Shomary Kapombe, Mohammed Hussein ‘Zimbwe’, Joash Onyango na Pascal Wawa.

 

 

Viungo wakiwa Thadeo Lwanga, Mzamiru Yassin na Larry Bwalya huku washambuliaji wakiwa ni Chris Mugalu, Luis Miquissone na Clatous Chama wakitumia mfumo wa 4-3-3.

 

 

Achana na kikosi hicho ambacho kimeweka historia ya kuisaidia Simba kuongoza kundi lake kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, pia kuna kile cha kipa Beno Kakolanya, mabeki David Kameta ‘Duchu’, Gadiel Michael, Kennedy Juma na Erasto Nyoni.

 

 

Hapo viungo watakuwa Jonas Mkude, Hassan Dilunga, Perfect Chikwende na Bernard Morrison na washambuliaji Meddie Kagere na John Bocco wakitumia mfumo wa 4-4-2. Vipi Yanga wanatokaje hapo?

 

 

Wakati ukifikiria vikosi hivyo viwili hatari vyote vikiwa ni nondo kwelikweli, bado kuna orodha ya nyota wengine nane wanabaki pembeni ambao wanahitaji sehemu chache tu wakamilishe kikosi na wacheze.

 

 

Kikosi hicho cha mwisho kinaundwa na wachezaji, kipa Ally Salim, Ibrahim Ame, Ibrahim Ajibu, Francis Kahata, Mnigeria Junior Lokosa, Mzimbabwe Peter Muduhwa, Said Ndemla na Miraji Athuman ‘Sheva’.

 

 

Sasa ukitaka kuwapangia kikosi chao hawa kwa kujumlisha na wachezaji wachache katika vikosi vya awali, kipa atakuwa ni Ally Salim, mabeki Duchu, Gadiel, Ame na Muduhwa, viungo Mzamiru, Ndemla, Kahata na Miraji, washambuliaji Lokosa na Ajibu.

 

 

Kwenye mchezo wa kwanza baina ya timu hizo uliopigwa Novemba 7, mwaka jana, walitoka sare ya kufungana bao 1-1 katika Uwanja wa Mkapa huku ule wa pili ukiwa Mei 8, 2021 uwanjani hapo.

SAID ALLY, Dar es Salaam

Leave A Reply