CCM Yaita Wanachama Wenye Sifa Kugombea Ubunge wa Afrika Mashariki
Chama Cha Mapinduzi kinapenda kuwajulisha wanachama wake wote, walio na nia na sifa za kuweza kugombea na kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki kwamba, mchakato wa kuchukua na kurejesha fomu za maombi ya kuteuliwa kugombea kwa ajili ya kujaza nafasi hiyo kupitia CCM, utaanza tarehe 10 Agosti 2024 na kumalizika tarehe 15 Agosti 2024.