GSM Wamzuia Saido Kuondoka Yanga

WAKATI mkataba wake ukielekea ukingoni, nyota wa Yanga, Mrundi, Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’ amezuiwa kuondoka na mabosi wa timu hiyo na kumtaka wakae chini kujadili kuongezewa mkataba wa kuendelea kukitumikia kikosi hicho.


Saido ambaye mkataba wake
unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu, amekuwa na kiwango kizuri msimu huu ambapo tayari amefunga mabao matatu kwenye Ligi Kuu Bara.


Mtu wa karibu na nyota huyo
fundi wa mipira iliyokufa ikiwemofaulo na penalti, ameliambia Spoti Xtra kuwa: “Ntibazonkiza anamaliza mkataba na Yanga mwishoni mwa msimu huu na mpaka sasa hajasaini mkataba mpya.

 


“Viongozi waliposikia kuwa ana
mpango wa kuondoka baada ya kupata ofa Uarabuni, wakaamua kukaa naye kikao ila inaonekana kama anataka fedha nyingi ambazo Yanga hawawezi kuzitoa.


“Baada ya mazungumzo ya
kwanza kushindikana, ndipo GSM (Gharib Said Mohamed, mdhamini wa Klabu ya Yanga) akamtafuta na kutaka amsubiri mpaka arejee nchini ili waweze kukaa na kuzungumza kuhusu suala hilo.

 


“Kila mtu anaona kiwango
chake ndiyo maana hata hizo timu zikamtafuta na kama Yanga hawatampa mkataba mapema basi anaweza kuondoka maana ofa za Uarabuni huwa ni kubwa sana.”

 

Alipotafutwa Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli, alisema: “Kwa sasa nipo bize, nitafute baadaye.” Alipotafutwa baadaye hakupatikana.

STORI: CAREEN OSCAR NA LEEN ESSAU

MORRISON Amtibua PABLO, HITIMANA OUT SIMBA, MSHAHARA wa KIPA YANGA KUFURU | KROSI DONGO….705
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment