Guardiola Alia na UEFA, FIFA

BOSI wa Manchester City, Pep Guardiola amelalamika kuwa Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) pamoja na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) yanachangia kuua vipaji vya wachezaji kutokana na ratiba kuwa ngumu.

 

Man City mpaka sasa msimu huu wapo katika michuano minne tofauti ambayo inaifanya timu hiyo kuwa bize.Timu hiyo inashiriki Premier, Ligi ya Mabingwa Ulaya, Kombe la FA na imefika fainali katika Carabao Cup.

 

Leo Jumanne, Man City itakuwa katika Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ikicheza dhidi ya Borusia Dortmund. Guardiola amekuwa akifanya mabadiliko katika kikosi chake ili kupunguza kuwachosha wachezaji hao kutokana na majukumu waliyo nayo.

 

“UEFA na FIFA zinawaua wachezaji wangu kwa kweli kutokana na ratiba kubana na aina ya michuano ambayo tunayo

“Tumekuwa hatuna mapumziko, kumbuka wachezaji ni binadamu na siyo mashine. Ndiyo maana unakuta nafanya mabadiliko kwa kila mchezo kwa wachezaji sita mpaka saba ili wawe fiti bila hivyo ni kazi.

 

“Unakuta mchezaji kama Rodri mpaka sasa amecheza mechi 42 tu kwa msimu huu, pia kuna wachezaji wao wanataka kucheza kila mchezo katika michuano yote na hapo ndiyo unakuwa mtihani zaidi wanatakiwa kuangalia hili.

Toa comment