The House of Favourite Newspapers

Guardiola Kubaki Etihad Hadi 2025, Aongeza Mkataba Mpya wa Miaka Miwili

0
Kocha wa Manchester City Pep Guardiola akiwa na mshambuliaji wa klabu hiyo raia wa Norway Erling Braut Haaland

KOCHA mkuu wa klabu ya Manchester City ya nchini Uingereza, Mhispania Pep Guardiola ameongeza mkataba mpya wa miaka miwili utakaomfanya kuendelea kuhudumu katika viunga vya Etihad hadi mwaka 2025.

 

Akiwa na Manchester City kocha huyo ameiongoza klabu hiyo katika michezo 374 akifanikiwa kushinda michezo 271, michezo 49 ikitoka sare na kupoteza jumla ya michezo 54.

Pep Guardiola ameongeza mkataba wa miaka 2 kuendelea kubaki Etihad

“Hii ni kuthibitisha tu ni kwa namna gani mimi na klabu tupo sawa katika mazingira ya kazi, sijui nishukuru namna gani kwa klabu kuendelea kuniamini na kunitengenezea mazingira mazuri ya kazi.” alisema Guardiola mara baada ya taarifa rasmi kutoka.

 

Kwa sasa Manchester City ipo katika nafasi ya pili ya msimamo wa Ligi Kuu ya NBC ikiwa na jumla ya alama 32 alama tano nyuma ya vinara Arsenal huku Ligi ikiwa imesimama kwa muda kupisha mashindano ya Fainali za Kombe la Dunia yanayoendelea nchini Qatar.

Leave A Reply