Gumzo la Faru Rajab Mtoto wa Faru John, Lazima Ucheke!

NINAAMINI utakuwa unamkumbuka Faru John, mnyamapori aliyekufa katika hifadhi ya Sasakwa Gruneti kwa kukosa matibabu alipoumwa.   Faru huyo aliacha mtoto aliyeitwa Faru Rajab ambaye amezua gumzo mitandaoni kutokana na taarifa zake mbalimbali.

 

Baadhi ya wadau wanahoji kwa nini Faru huyo aitwe Rajab wakati ametoka katika uzao wa Faru John, ina maana ‘wazazi wake walibadili dini?’ Gumzo kubwa zaidi ni zile taarifa za hivi karibuni za Hifadhi ya Serengeti nchini Tanzania kumpongeza Faru Rajab kwa kuongeza idadi ya faru katika hifadhi hiyo.

 

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamis Kigwangalla,  ameingilia kati mjadala huo na kuahidi kufuatilia sababu ya mtoto wa Faru John kuitwa Faru Rajab.    Amesema huenda faru Rajab alibadili dini baada ya kuoa au amefuata dini ya mama yake baada ya baba yake Faru John kufa.

 

Kifo cha Faru John kilizua hali ya sintofahamu na Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa, aliunda kamati kwa ajili ya uchunguzi. Akiwasilisha ripoti hiyo kwa Majaliwa mwaka 2017, Profesa Samwel Mnyele alisema Daru John alikosa matunzo na uangalizi wa karibu.

 

Mnyele alisema hakukuwa na kibali rasmi cha kumhamisha Faru John kutoka Hifadhi ya Ngorongoro kwenda Gruneti. Alisema kamati hiyo imeshauri hatua za kiutawala zichukuliwe dhidi ya ofisi ya Mkurugenzi wa Wanyamapori na Mhifadhi wa Hifadhi ya Ngorongoro kutokana na mapungufu yaliyojitokeza. Majaliwa alipongeza kamati hiyo na kusema serikali itayafanyia kazi mapendekezo ili kulinda maliasili.

TAZAMA TUKIO HAPA


Loading...

Toa comment