Gwajima Apiga Marufuku Waombolezaji Kulia Msiba wa Mama Yake – Video

ASKOFU wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Dk. Josephat Gwajima ameacha gumzo na mshangao baada ya kuzuia watu kulia kwenye ibada ya kuaga mama yake mzazi, Bi. Ruth Paulo Gwajima iliyofanyika nyumbani kwa mchungaji huyo na kisha mwili wa marehemu kuzikwa kwenye shamba la familia, nje kidogo na nyumbani hapo, Salasala jijini Dar.

Mama mzazi wa Gwajima alifariki Jumapili ya wiki iliyopita baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa kansa kwa muda mrefu. Marehemu ameacha mume, watoto 11 wajukuu na vitukuu.

GWAJIMA: “Marufuku Kulia Kwenye Msiba wa Mama Yangu”

Toa comment