The House of Favourite Newspapers

GWAJIMA ATINGA IKULU, ASHUSHA MAOMBI MAZITO MBELE YA JPM – VIDEO

ASKOFU wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Dkt. Josephat Gwajima, leo Jumatano, Desemba 12, 2018 amekuwa miongoni mwa wageni walioalikwa Ikulu jijini Dar es Salaam kushuhudia Rais John Magufuli  akisaini mkataba wa mradi wa kufua umeme wa Stiegler’s Gorge katika Mto Rufiji.

 

Akifanya maombi mafupi kabla ya kuanza kwa hafla hiyo, ambapo mkandarasi wa mradi huo anatoka Misri na serikali ya Tanzania, Gwajima aliwaombea kwa Mungu awawezeshe  nguvu wote wanaofanya kazi na Rais John Magufuli, Makamu wa Rais, Samia Suluhu;  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa;  mawaziri na watumishi wote wa serikali.

 

“Nafunga kila kazi zenye kukwamisha mradi wa Stiegler’s Gorge, ukiwemo wizi, rushwa, maneno ya kuvunja moyo; nayazuia katika jina la Yesu na kila mmoja katika nafasi yake atiwe nguvu,” alisema katika sala yake, akiwa miongoni mwa viongozi kadhaa wa madhehebu ya Kikristo na Kiislam waliotoa sala zao.

 

VIDEO: FUATILIA TUKIO HILO HAPA

Comments are closed.