The House of Favourite Newspapers

Gwajima, Flora kumlipa mamilioni Mbasha!

0

mbashaaaa.jpgMwimbaji nyota wa muziki wa Injili Bongo, Flora Mbasha.

Stori: Mayasa Mariwata

MCHUNGAJI Kongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima na mwimbaji nyota wa muziki wa Injili Bongo, Flora Mbasha watalazimika kumlipa mamilioni ya shilingi Emmanuel Mbasha (33) kwa kitendo chao cha kumchafulia jina mbele ya jamii, Risasi Mchanganyiko limeelezwa.

Hivi karibuni, Emmanuel ambaye ni mume wa Flora, alishinda kesi ya ubakaji iliyofunguliwa dhidi yake katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini Dar akidaiwa kumbaka mdogo wa mkewe waliyekuwa wakiishi naye nyumbani kwao, Tabata, Dar es Salaam, Juni 2014.

Katika shauri hilo, Mbasha alishitakiwa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (mlalamikaji anakuwa shahidi), kitu kinachoibua maswali ni kwa namna gani Gwajima na Flora watahusishwa.

gwajima001.jpg
Mchungaji Kongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima

GWAJIMA, FLORA WANAHUSIKAJE?

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko jijini Dar juzi, Mwanasheria na Ofisa wa Mahakama Kuu, Denis Maringo alisema mazingira ya kesi hiyo iliyokuwa gumzo kubwa, yanawaingiza wawili hao katika madai ambayo Mbasha anaweza kufungua kwani kuna uhusiano unaojitosheleza kati yao na binti anayedai kubakwa.

“Inafahamika kwamba aliyedai kubakwa ni mdogo wake Flora na kwa kipindi chote kile cha kesi, inafahamika pia kuwa Flora alikuwa karibu na Mchungaji Gwajima, maana mara nyingi zilisikika kauli za Mbasha kulalamika nyendo za mchungaji na mkewe.

“Kuna wakati Mbasha alidai kuwa, alikwenda kwa Mchungaji Gwajima ili kupata muafaka wa tatizo lake na mkewe, lakini akasema kiongozi huyo wa kiroho alimwambia kama mkewe ameshaamua, ni vizuri akaheshimu uamuzi wake. Hii inaonesha ukaribu wa wawili hao,” alisema mwanasheria huyo.

ema-mbashaEmmanuel Mbasha.

KWA NINI MBASHA ASHITAKI?

Mwanasheria huyo alisema kuwa, Mbasha anaweza kufungua shauri la madai na kuomba fidia ya mamilioni ya fedha kutokana na heshima yake kwa jamii kushuka na kuchafuka, hasa kwa kulinganisha na umaarufu alionao katika jamii.

“Kesi ya ubakaji inamshushia mtu thamani katika jamii, hivyo kutokana na adha hiyo, pale unapokutwa huna hatia na mahakama unaruhusiwa kufungua kesi ya madai kwa lengo la kutaka fidia kiasi unachokitaka na mahakama kukitolea uamuzi kwa kumshitaki mhusika na wote walioshiriki katika kesi hiyo.

“Anachopaswa kufanya Mbasha ni kwenda Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam ambayo ni tofauti na ile ya awali iliyoendesha mashitaka na kufungua kesi ya madai ambapo sheria ya mwaka 1971 inaruhusu mtu kufungua kesi ya aina hiyo kwa kipindi kisichozidi miaka mitatu tangu hukumu itolewe. Kwa sababu ya kudhalilishwa, atawashitaki waliomshitaki mwanzo kwa kesi ya jinai.”

SHERIA INASEMAJE?

Wakili huyo alichambua vipengele  vinavyompa urahisi Mbasha wa kufungua kesi hiyo kuwa ni kile kinachohusu nia mbaya ya mfungua kesi akiwa na lengo la kumchafua.

“Mtu akikufungulia kesi kwa nia mbaya ya kukuchafua wewe. Kwa hiyo, yeye na walioshirikiana naye, wote wanahusika. Kipengele kingine ni kile cha adha ya kuwekwa ndani. Kwa kuwa mahakama ilimkuta hana hatia, maana yake ni kwamba, kitendo cha kuwekwa ndani ni cha uonevu unaoweza kuwaingiza matatani hata polisi wenyewe.

“Jambo lingine linalompa nafasi Mbasha ya kufungua madai ni kwa kitendo cha jamii kumuona tofauti kiasi kwamba inaweza kumtenga kwa kuamini ni mbakaji. Ili kuwa fundisho kwa watu wengine, anayo haki ya kudai fidia kwa kuchafuliwa jina kwani huenda hiyo iliwafanya wahusika kunufaika kwa dhamira zao.”

Wakati ishu hiyo ikionekana kuwakalia vibaya Mchungaji Gwajima na Flora, gazeti hili lilimtafuta Mbasha  ambaye baada ya kuelezwa kuhusu maelekezo ya mwanasheria huyo, aliomba muda wa kutafakari pamoja na wanasheria wake.

“Ni kitu kipya unanieleza na kama unavyojua hili ni suala la kisheria. Siwezi kulitolea maelezo mara moja, inabidi kukutana na kushauriana na wanasheria wangu ili kuona nini tunaweza kufanya,” alisema Mbasha.

Flora na Gwajima nao walitafutwa kupitia simu zao za mkononi, lakini mara zote hazikuweza kupatikana hadi gazeti hili lilipokwenda mtamboni. Hata hivyo, jitihada za kuwatafuta bado zinaendelea.

Leave A Reply