The House of Favourite Newspapers

#GlobalMusic: H_Art The Band x Lady JayDee Waachana Njia Panda Safari Ya Mapenzi Kwenye ‘Rosella’ – (Video)

Kwenye zile zinazotrend wekeend hii kutoka East Africa ni pamoja na hii ya H_Art The Band kutoka Kenya na Malkia wa Bongo Fleva Lady JayDee.

H_Art The Band kutoka Kenya na Lady JayDee wameshirikiana kutuletea wimbo wao mpya ‘Rosella’ ambayo video yake imeongoza na Kevin Bosco Jnr.

‘Rosella’ ni wimbo unaosimulia stori  ya mapenzi kati ya watu wawili waliobaki njia panda.

Akiwa muoga wa kueleza hisia zake, Rosella anabaki kuumia akitamani yule ampendaye ajue kile kilichopo moyoni mwake, akiendelea kujiuliza kama kweli jamaa kabadilika… Lakini hata kama angekuwa na ujasiri wa kufanya hivyo, mwanaume huyo ana sababu zinazomfanya afikirie tofauti na pengine kujuta na kukata tamaa juu ya penzi hilo licha ya kuwa bado anampenda sana mrembo huyo.

Watazame na sikiliza stori za pande zote mbili kwenye hizi dakika tano hapa chini.

H_Art The Band x Lady JayDee – ‘Rosella‘ 

Ushawahi kuachwa au kubaki njia panda mdau kwenye mapenzi? Tubonge kwenye comments.

 

Imeandikwa Na: Sandra Brown.

Subscribe kwenye YouTube Chanel yetu ya Global TV Online ili zote kali zinazotufikia iwe ni siasa, michezo, comedy, burudani, stori za mastaamuziki na nyingine zikufikie kwa wakati.

Comments are closed.