H-Baba Apandisha Mzuka Singeli Festi

KUELEKEA Tamasha la Singeli Festi litakalofanyika Oktoba 31, mwaka huu, Msanii wa Bongo Fleva, Khamis Ramadhan ‘H-Baba’ ameongeza mzuka baada ya kuwa miongoni mwa wasanii 22 watakaokuwepo.
Tamasha hilo ambalo linatarajiwa kufanyika Rongoni Beach, Kigamboni, Dar, linadhaminiwa na Global TV, Spoti Xtra na +255 Global Radio.
Akizungumza na Spoti Xtra, Mratibu wa Singeli Festi, Masoud Kandoro, alisema: “Mpaka sasa tuna wasanii 22 watakaoshiriki ambao ni Kinata MC, Balaa MC, Msaga Sumu, Man Fongo, Mzee wa Bwax, Meja Kunta, Dullah Makabila, Dogo Elisha, Seneta, Mimah, Vairas Mdudu, Lau Nation, Mackzube, PK MR. Konk, Six Bullet, Mczo Morfani, Dogo Toma, Dakota Mtu Hatari, Nicky Nyashy na Buda zoni.
“Pia H-Baba ameongezeka kwenye idadi ya wasanii watakaokuwepo kwa ajili ya kuongeza mzuka wa tamasha hilo.”
LEEN ESSAU

