The House of Favourite Newspapers

Habari Njema kwa Vijana Wenye Vipaji vya Public Speaking

0

KAMA wewe ni kijana na una kipaji cha kunena mbele za watu kwa lugha nyingine (PUBLIC SPEAKER) basi usikubali kupitwa na fursa hii ya kushiriki kwenye Shindano la National Public Speaking Competition.

 

Mratibu wa shindano hilo, Pacific Ibrahim, tarehe ya mwisho ya kuchukua na kurejesha fomu kwa ajili ya kushiriki Shindano hilo imesogezwa mbele hadi Februari 7, 2020 na zoezi la usaili litafantika Februari 10, 2020.

 

Mchujo utafanyika wa kuwapata vijana 30 ambao watapewa mafunzo maalum na baadaye kuchuana vikali, kuwatafuta washindi watatu ambao watajinyakulia zawadi ya shilingi milioni 10, mshindi wa kwanza akipata shilingi milioni 5, mshindi wa pili akipata shilingi milioni 3 na mshindi wa tatu akipata zawadi ya shilingi milioni 2.

 

Washiriki wa shindano hilo, watapata fursa ya kunolewa na waalimu wabobezi wa ‘public speaking’ katika shindano hilo.

 

Walengwa ni vijana wote wa Kitanzania wenye umri wa kati ya miaka 18 – 30, wenye ndoto za kuja kuwa wazungumzaji mbele ya halaiki. Amesema fomu hizo zinatolewa katika ofisi za Global Group, Sinza Mori jijini Dar na kwenye vyuo vyote nchini.

 

Fomu za kujiunga ni Tsh 5,000/-. Kwa mawasiliano zaidi: 0672881723
@lydia_sahan.

KWA MIKOANI FOMU ZINAPATIKANA KWA MAWAKALA WA GLOBAL PUBLISHERS

TANGA MJINI
MAHALI: BARABARA YA 15
NAMBA: 0715469495- Christopher Haule

MBEYA
NAMBA: 0754-891019 Lalika Mohamed
MAHALI: UPA Jengo Linalotazamana na POSTA ( NHC- INTERPRIVE HALL)

ARUSHA
NAMBA: 0715-839470
Khalifa Adam
MAHALI: JENGO LA CCM

MOROGORO
NAMBA: 0655485179
Abu Nasib Nassor
MAHALI: Manispaa Ya Morogoro TRA

MWANZA
NAMBA: 0745338940
Johnson James.

 

Leave A Reply