Kero ya Maji Kishapu Shinyanga
WAKATI nchi yetu Tanzania ikiadhimisha wiki ya maji, imeelezwa kuwa wanawake wengi wilayani Kishapu mkoani Shinyanga wamekuwa wakitumia muda mwingi kutafuta maji hivyo kushindwa kushiriki katika shughuli za maendeleo kikamilifu.
Akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea wilayani humo wananchi wa vijiji vya Nyenze na Ng’wang’holo kata ya Mwadui Lohumbo wilayani humo walisema maji ni changamoto kubwa inayorudisha nyuma maendeleo ya wananchi kwani wanatumia muda mwingi kutafuta maji.
Msemaji huyo alifungukua kuwa licha ya kuishi karibu na mgodi wa almasi wa Williamson bado wanalazimika kutembea umbali takribani kilomita tano kufuata maji katika mto Tungu unaotenganisha wilaya ya Kishapu na wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu.
Comments are closed.