Ilipoishia Sehemu ya 4
Hakukuwa na siri tena, kila kitu kilijulikana, mkewe alijua kila kitu kilichotokea hali iliyompa wakati mgumu mno moyoni mwake. Hakuwa na cha kufanya zaidi ya kumuomba msamaha mke wake.
“Naomba unisamehe mke wangu!” alisema Edson huku akimwangalia mkewe usoni.
“Usijali mume wangu! Nimekusamehe hata kabla hujaniomba msamaha,” alisema Rachel pasipo kumwambia mumewe kwamba huyo Stela alikuwa amefariki dunia. Kama yeye alikuwa hivyo, vipi kuhusu Stela? Alitamani kuuliza lakini akaona bora kunyamaza kwa kuona kwamba angemuumiza mke wake.
SONGA NAYO…………..
“Abraham, upo wapi?”
“Nipo saluni nanyoa!”
“Wapi?”
“Sinza.”
“Naweza kukuona leo?”
“Leo? Saa ngapi?”
“Baada ya saa moja. Kuna kazi nataka nikupe..”
“Sawa bosi! Nitakuja. Nyumbani au ofisini?”
“Njoo ofisini!”
“Bado hujasepa tu?”
“Bado! Leo mpaka usiku!”
“Sawa mkuu!”
Boniface alikuwa akizungumza na rafiki yake kwenye simu aliyeitwa Abraham, alikuwa miongoni mwa vijana aliokuwa akifanya nao kazi kubwa, kila alipokuwa na kazi nyeti, alikuwa akimtumia kwa ajili ya kuyaweka mambo yake sawa.
Kipindi hicho alikuwa akizungumza naye, alitaka kuonana naye kwa sababu kulikuwa na kazi kubwa alitaka kumpa. Hakutaka kumwambia kazi gani na hata Abraham hakutaka kuuliza hilo kwani siku zote hakuwa muulizaji mpaka pale alipokuwa akipewa kazi tena kwa malipo makubwa.
Wakati akipigiwa simu ndiyo kwanza ilikuwa saa kumi na mbili jioni. Alishangaa sana, hakuwahi kupigiwa simu na Boniface wakati kama huo kwani kazi zake nyingi zilifanyika mchana, kitendo cha kupigiwa simu muda huo na kuambiwa kwamba walitakiwa waonane baada ya saa moja, ilimpa maswali mengi mno.
Hakutaka kujiuliza sana, alimwamini Boniface kwamba hakuwa mtu wa matukio mabaya, kama alivyoambiwa kwamba alitakiwa kwenda kumuona kwa ajili ya kumpa kazi hiyo, akakubaliana naye.
Saa moja na nusu usiku akafunga safari na kuelekea Posta Mpya. Alipofika ofisini kwa Boniface, akaambiwa aingie ndani ambapo akamkuta Boniface akichungulia dirishani kama kawaida yake, alikuwa akimwangalia Miriam aliyekuwa sehemu yake ya kulala usiku huo.
Moyo wa Boniface ulimuonea huruma, hakukuwa na kitu kilichokuwa kikimuumiza moyoni mwake kama kumuona msichana huyo mwendawazimu alivyokuwa akiteseka, alijua kwamba hakuwa na ufahamu juu ya kile kilichokuwa kikiendelea lakini hakutaka kumuona akiteseka vile.
“Nimefika…” alisema Abraham mara baada ya kuingia ndani ya ofisi ile.
“Karibu sana Abraham. Hebu sogea hapa dirishani,” alimkaribisha Boniface na kumtaka Abraham amsogelee kule dirishani alipokuwa amesimama. Akafanya hivyo.
“Unamuona yule msichana mrembo?” aliuliza Boniface.
“Yupi? Mbona simuoni mtu!”
“Yule aliyelala pale chini!”
“Miriam Mwendawazimu?”
“Unakosea kumuita hivyo! Sema Miriam tu inatosha…” alisema Boniface, jina aliloliita Abraham lilimuumiza moyoni mwake.
“Ndiyo! Nimemuona!”
Alichokifanya Boniface ni kuanza kumuhadithia namna alivyokuwa akimpenda Miriam Mwendawazimu. Hakutaka kumficha kwani kazi kubwa aliyotaka kumpa ilikuwa ni juu ya yule mwendawazimu.
Abraham akapigwa na mshangao, hakuamini kile alichoambiwa kwamba Boniface alikuwa akimpenda sana mwendawazimu huyo na alikuwa tayari kufanya chochote kile kwa ajili yake mpaka kuhakikisha anakuwa wake.
“You are kidding, right?” (unatania, si ndiyo?) aliuliza Abraham huku akitoa tabasamu.
“Abraham, I’m serious, can you do me a favor?” (Abrahm, ninamaanisha, unaweza kunisaidia?) aliuliza Boniface.
Abraham hakujibu kitu, kwanza akabaki kimya huku akimwangalia bosi wake. Alikuwa mwanaume mwenye pesa, aliyekuwa akinyenyekewa na wanawake wengi, sasa iweje aanze kumpenda mwendawazimu?
Hiyo haikumuingia akilini hata kidogo. Wakati mwingine alihisi kama bosi wake huyo alikuwa akimtania tu kwani alifikiria idadi ya warembo waliokuwa wakimpenda lakini mwisho wa siku kusema kwamba alimpenda Miriam Mwendawazimu, hiyo haikuingia akilini.
“Lakini bosi…”
“Abraham, ninataka unisaidie kazi!”
“Kazi gani?”
“Ninampenda sana Miriam kama nilivyokwambiia. Ninahitaji kitu kimoja tu. Kuzaa naye,” alisema Boniface huku akimwangalia Abraham.
“Unasemaje?”
“Nadhani umenielewa. Ninataka kuzaa na Miriam haraka iwezekanavyo!”
Boniface alimaanisha, alimwambia namna ambavyo angezaa na msichana huyo. Ilikuwa ni lazima afanye naye mapenzi. Akampa njia ya kufanya mapenzi na Miriam kwamba ilikuwa ni lazima wamchukue na kuelekea naye sehemu fulani, huko, angefanya mapenzi na kichaa huyo kwenye gari.
Ulikuwa mpango mchafu lakini hakuwa na jinsi, ilikuwa ni lazima mpango huo ufanyike na afanye mapenzi na msichana huyo. Hakujali kama alikuwa mwendawazimu, kitu ambacho alikitaka moyoni mwake ni kufanya kile alichokitaka tu.
“Upo tayari tukamchukue?” aliuliza Boniface.
“Sawa mkuu!”
“Ila kumbuka, kila kitu kitakachotokea leo na siku nyingine kiwe siri. Umenielewa?” aliuliza Boniface.
“Ndiyo bosi!”
“Basi sawa! Ngoja tusubiri mpaka saa tano usiku tukamchukue,” alisema Boniface. Hilo halikuwa na tatizo lolote, wakakubaliana na hivyo kuanza kusubiri muda wa kazi ufike na Boniface kufanya mapenzi na Miriam Mwendawazimu.
Comments are closed.