The House of Favourite Newspapers

Hadithi: Insane (Mwendawazimu -6)

Ilipoishia Sehemu ya 5

“Ndiyo bosi!”
“Basi sawa! Ngoja tusubiri mpaka saa tano usiku tukamchukue,” alisema Boniface. Hilo halikuwa na tatizo lolote, wakakubaliana na hivyo kuanza kusubiri muda wa kazi ufike na Boniface kufanya mapenzi na Miriam Mwendawazimu.

Sasa Endelea…

Hawakutaka kuchelewa, walichokifanya ni kupanga namna ya kumchukua Miriam Mwendawazimu huyo na kuondoka naye. Hiyo haikuwa kazi kubwa, ni kweli walikuwa na mpango wa kumteka lakini lisingewafanya watu kuwa na hofu nao au hata kuwaingiza matatani kwa sababu mtu aliyetakiwa kuchukuliwa alikuwa mwendawazimu.

Macho yao yalikuwa kwenye saa zao tu, kwa Boniface, aliona mshale wa dakika ukienda taratibu sana huku rafiki yake, Abraham akiwa na maswali mengi kichwani mwake juu ya kile kilichotakiwa kufanywa.

Bado hakujua ni kitu gani kilimsibu rafiki yake huyo. Haikumuingia akilini kuona kama kungekuwa na mtu aliyekuwa ambaye angetamani kufanya mapenzi na mwendawazimu kwa sababu tu alimpenda. Wakati mwingine alimuona Boniface kama mtu aliyechanganyikiwa, kwani kupanga uamuzi kama ule halikuwa jambo la kawaida hata kidogo.

“Abraham. Naomba suala hili liwe siri kati yangu na wewe,” alisema Boniface huku akimwangalia Miriam aliyekuwa kule chini.

“Hakuna tatizo bosi! Kwenye kutunza siri wala usijali!”

Waliendelea kusubiri mpaka ilipofika saa tano usiku ndipo wakatoka ndani ya ofisi hiyo. Jengo zima hakukuwa na watu wengine zaidi yao na baadhi ya walinzi waliokuwa wakililinda jengo hilo.

Moja kwa moja bila kuzungumza na mtu mwingine yeyote, wakaondoka na kuingia ndani ya gari aina ya Noah na kuondoka mahali hapo. Hawakutaka kumfuata Miriam moja kwa moja bali walichokifanya ni kujifanya kama walikuwa wakienda Feri, huko mbele wakageuza na kuanza kurudi kule walipotoka ili kuwafanya watu wasijue kama wao ndiyo waliokuwa wakifanya mchezo huo.

Boniface alikuwa makini kwenye usukani wa gari lake, ni kweli alijua kwamba kile alichotaka kukifanya kilikuwa kibaya lakini hakuwa na jinsi, ilikuwa ni lazima afanye hivyo kwani kama kupenda, moyo wake ulikuwa umefika kiwango cha mwisho kabisa cha kupenda.

Wakati akiendesha kuelekea kule alipokuwa Miriam, simu yake ikaanza kuita, alipoangalia, alikuwa ampenzi wake, Jesca. Hakutaka kupokea simu hiyo, moyo wake ulikuwa kwa mtu mmoja tu, Miriam Mwendawazimu, aliona kama ile simu ingemzingua.

Walipofika alipokuwa Miriam, Abraham akaufungua mlango na kutoka. Hakutaka kuangalia huku na kule kwani aliamini kwamba hakukuwa na mtu yeyote yule. Alichokifanya ni kumfuata Miriam, akamuamsha, alipoamka tu, akamchukua kinguvu na kuanza kumpeleka kwenye gari.

Ilikuwa vurugu, Miriam hakutaka kukubali, alileta vurugu, purukushani za hali ya juu kutaka kujitoa mikononi mwa Abraham lakini hilo lilishindikana kutokana na nguvu kubwa alizokuwa nazo mwanaume huyo. Akamuingiza ndani ya gari na haraka sana Boniface kuliondoa gari hilo mahali hapo.

“Twende wapi sasa?” aliuliza Abraham.

“Jangwani!” alijibu.

Safari ya kwenda Jangwani ikaanza. Njiani hawakutaka kusimama, Miriam alikuwa akileta fujo ndani ya gari lakini hakuweza kusababisha madhara yoyote yale kwa Abraham ambaye alimshikilia vilivyo.

“Subiri nije mimi,” alisema Boniface huku akisimamisha gari na kuanza kuvua nguo zake kabisa.

“Nishaona kama tukisimamisha gari njiani, watu watatushtukia, cha msingi endesha gari mimi nimalize kazi yangu,” alisema Boniface huku akiingia kule nyuma.

Hilo halikuwa tatizo, yeye akamshikilia Miriam na kisha Abraham kuelekea kushikilia usukani. Haikuwa kazi nyepesi kumbaka Miriam, nyuma ya gari kulikuwa na purukushani kubwa.

Huku Boniface akiwa na boksa tu, alijitahidi kuleta kila aina ya purukushani ilimradi afanikishe kile alichokuwa akikitaka. Ilifika kipindi Miriam alichoka, akaamua kuacha na lolote lile na hapo ndipo Boniface alipokamilisha mchakato wake wa kufanya mapenzi na Miriam Mwendawazimu.

Miguno ikaanza kusikika nyuma ya gari, haikuwa kwa Boniface tu bali hata kwa Miriam mwenyewe. Kilikuwa kitendo cha kikatili lakini kitu cha ajabu, Miriam ndiye ambaye akaanza kumng’ang’ania Boniface na kumvutia kwake.

Kitendo hicho kilichukua dakika kumi, tena huku gari likipita Magomeni, Manzese, Shekilango mpaka Sinza, likapitiliza mpaka Mwenge na kuanza kurudi Posta kwa kutumia Barabara ya Ali Hassan Mwinyi.

“Hapa nimeridhika! Huyu mrembo lazima nizae naye,” alisema Boniface wakati wakifika katika sehemu ile ile waliyomtoa Miriam na kumuacha mahali hapo na wao kuondoka.

Huo ndiyo ulikuwa mchezo wao. Mara kwa mara walikuwa wakimchukua Miriam na kuondoka naye. Siku ya kwanza ilikuwa ni kwa nguvu lakini siku ya pili na nyinginezo, Miriam mwenyewe alikuwa akifurahi kila alipoliona gari lile limesimama karibu yake, tena wakati mwingine kulifuta na kutaka kuingia ndani.

Huyo akawa msichana mpya wa Boniface, ndiye msichana aliyekuwa akimfurahisha motoni mwake, ndiye msichana aliyemteka na kuwaona wengine kuwa si lolote lile.

Wakati hayo yote yakiendelea, msichana wake, Jesca alikuwa kwenye wakati mgumu, hali ilikuwa mbaya na uhusiano ulikuwa ukiyumba kila siku. Msichana huyo alikosa furaha, mapenzi motomoto aliyoyapata kipindi cha nyuma yakapotea kabisa.

Alihuzunika, hakutaka kukubali, alichokifanya ni kuwaita wazazi wa pande zote mbili na kuwaambia kilichokuwa kikiendelea. Hakujua kama mpenzi wake alikuwa amempata mpenzi mwingine. Alimchunguza na kumchunguza lakini hakuwa amegundua kitu chochote kile.

“Mpaka nimewaita, sijajua kinachoendelea, Boniface amebadilika, si kama zamani,” alisema Jesca huku akiwaangalia wazazi hao, wote walikuwa kwenye kikao kidogo.

“Tatizo nini Boniface?” aliuliza baba yake.

“Hakuna tatizo! Sina msichana yeyote yule. Simu yangu hii hapa, hakuna chochote kibaya,” alisema Boniface.

Ilikuwa kesi ndogo ambayo iliamuriwa na Boniface mwenyewe kwamba angebadilika na kumpenda mpenzi wake kama zamani. Hilo lilikuwa gumu kutokea, hakuweza kumpenda Jesca kama zamani, penzi la Miriam liliuteka moyo wake kiasi kwamba akawa haoni wala hasikii kwa lolote lile.

Baada ya kufanya mchezo huo kwa kipindi cha miezi sita, hatimaye alichokuwa akikitaka akaanza kukiona. Kupitia dirishani kwake ofisini, akaanza kumuona Miriam akianza kutapika mfululizo.

Hakutaka kujiuliza juu ya hilo lililokuwa likiendelea, moyo wake ukamwambia kwamba msichana huyo alikuwa mjauzito. Hakutaka kumuona mwendawazimu huyo akiteseka, akatoa taarifa katika kituo kimoja cha afya na hivyo msichana huyo kuchukuliwa.

“Ana mimba…” alijibu nesi aliyempima.

“Unasemaje?”
“Huyu Mwendawazimu ana mimba!”

“Acha masihara. Imekuwaje mpaka awe na mimba?”
“Kwa sababu amfanya mapenzi!”

“Yaani kuna mtu amelala naye! SI ndiyo?”

“Ndiyo!”

Si manesi walioshangaa, hata daktari alipoletewa ripoti na kuonyeshewa kwamba Miriam alikuwa na mimba alishangaa. Halikuwa jambo la kawaida kwa mwendawazimu kupata ujauzito.

“Jamani! Kweli watu ni mashetani! Yaani unafanya mapenzi na kichaa mpaka kumpa mimba! Hii ni roho ya kishetani!” alisema daktari, hakujua kwamba mtu aliyempa mimba mwendawazimu huyo ndiye yuleyule aliyemleta hospitalini hapo.

Kwa Boniface hicho ndicho alichokitaka. Alifurahi kuona amefanikiwa kumpa mimba Miriam, nyumbani, akaonekana kuwa na furaha kubwa kiasi kwamba hata mpenzi wake, Jesca ambaye mara kwa mara alikuwa akifika nyumbani hapo alishangaa kwani kwa kipindi kirefu mwanaume huyo hakuwa na furaha kabisa, muda mwingi alionekana kuwa na mawazo.

“Kuna nini tena?” aliuliza Jesca.

“Hakuna kitu! Nashangaa kujiona nikiwa na furaha hivi!” alijibu Boniface huku akikenua.

“Mmh! Naomba unishirikishe!”

“Niamini mpenzi! Hakuna kitu!”

Hakutaka kumwambia mtu yeyote yule, kila siku aliendelea kuwa na furaha tele moyoni mwake. Wakati mwingine alikuwa akimshukuru Mungu kwani alifanikiwa kumpa mimba mwanamke aliyekuwa akimpenda kwa mapenzi ya dhati kutoka moyoni mwake.

Wakati akijifikiria hilo, akaamua kupanga mikakati ya kumuacha Jesca, asingeweza kuendelea kuwa na msichana huyo na wakati upande wa pili kulikuwa na msichana mwingine, akahisi kama alikuwa akifanya mchezo mchafu wa kumsaliti Miriam.

“Bora nimuache huyu malaya Jesca, siwezi kumsaliti Miriam. Bora nimwambie ukweli kwamba kama mapenzi kufa, acha yafe sasa hivi nibaki nilee mimba na nisubiri mtoto,” alisema Boniface. Hakutaka kuchelewa, hapohapo akachukua simu yake na kumpigia simu Jesca.

Comments are closed.