HADITHI MPYA YA SHIGONGO: My Heart is Bleeding (Moyo Wangu Unavuja Damu)

NI hadithi mpya yenye kusisimua ambayo itakufundisha mambo mengi ya kuhusu maisha na mapito yake, itakuhitaji uwe mvumilivu na mwenye moyo mgumu kuzuia machozi yasikutoke maana hisia zako zitaguswa na moyo wako utageuzwa ndani-nje.  Washiriki katika hadithi hii ni:

 

Raymond Kijiko – Mwanafunzi wa chuo cha Usimamizi wa Fedha jijini Dar es Salaam, mtanashati, anayejisikia, mwenye sura nzuri na mwanasoka anayemvutia kila msichana anayemtazama, zaidi ya yote ni mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya ambapo jina lake maarufu ni  Ray D.

 

Joan  Ndyamkama – Msichana mrembo, mwenye asili ya Rwanda na Ethiopia, ambaye amewahi kuwa Miss Tanzania na hivi sasa ni mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha akisoma darasa moja na Raymond.  Anamtaka Raymond kwa udi na uvumba.

 

Shinje Mabula – Msichana mwingine mrembo kupindukia, Msukuma kutoka Mwanza, mwenyeumbile  la Kanda ya Ziwa, miguu ya bia, mrefu, kiuno chembamba na makalio ya kutosha!  Aliwahi kushinda taji la Miss Bantu kabla ya kujiunga na Chuo cha Usimamizi wa Fedha.  Yeye kama ilivyo kwa Joan anampenda Raymond na angetaka awe mpenzi wake.

 

Deborah Kashaija –  Kama ingetokea ukaita warembo kumi katika Afrika wasimame mbele yako, Deborah angekuwa miongoni mwao, alikuwa na kila sifa ya kuitwa mwanamke mrembo, laiti ungekutana naye  katikati ya usiku usingetimua mbio ukidhani ni jini!  Mama yake alikuwa Mwarabu mwenye asili ya Dubai lakini baba yake Mhaya kutokela Kanyigo, Bukoba.  Yeye pia anamtaka Raymond kwa gharama yoyote.

 

Haleluya Dito – Msichana mfupi mwenye miguu iliyopinda, kichwa kikubwa kilichojaa nundu, macho makubwa yaliyotoka nje na masikio marefu kuliko kawaida,ana sura mbaya ya kuweza kumfananisha na watu wa sayari nyingine!   Pia ni mwanafunzi wa IFM, anamtaka Raymond.

 

Ni ligi kubwa, je, nani atafanikiwa kummiliki kijana Raymond mwenye jina kubwa na fedha nyingi miongoni mwa  vijana nchini Tanzania, akiwa mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha?

Ifuatilie hadithi hii hadi mwisho upate kufahamu nani aliibuka mshindi, visanga, visa, visasi na mauaji ya kutisha yatatokea katika harakati za kumgombania Raymond.

 

FUATILIA HADITHI HII MPYA YA ERIC SHIGONGO KWENYE GAZETI LA SPOTI XTRA KESHO ALHAMISI, NOVEMBA 8, 2018.


Loading...

Toa comment