The House of Favourite Newspapers

Haji Manara Afutiwa Adhabu Ya TFF

0
Haji Manara.

 

KAMATI ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), chini ya mwenyekiti wake, Tarimba Abass, leo Jumatatu imefikia uamuzi wa kumfutia adhabu Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara.

Kamati hiyo imefikia uamuzi huo baada ya Manara kuomba kupitiwa upya adhabu aliyopewa hapo awali ya kufungiwa kutojihusisha na soka kwa kipindi cha miezi 12 na kulipa faini ya Sh milioni 9.

 

Kutokana na kufutwa kwa adhabu hiyo, Manara kuanzia leo atakuwa huru kuendelea kufanya majukumu yake ya soka ndani ya Simba.

Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu ya TFF, Tarimba Abbas akizungumza na wanahabari leo mchana ikiwa ni maamuzi waliyoyafikia ya kamati ya nidhamu na kuwafungulia baadhi ya wanafamilia wa mpira waliokuwa wamefungiwa kujihusisha na mpira ndani na nje ya nchi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu ya TFF, Tarimba Abbas akizungumza na wanahabari leo mchana ikiwa ni maamuzi waliyoyafikia ya kamati ya nidhamu na kuwafungulia baadhi ya wanafamilia wa mpira waliokuwa wamefungiwa kujihusisha na mpira ndani na nje ya nchi.

 

Mbali na Manara, kamati hiyo pia imewafutia adhabu Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Rukwa, Blassy Kiondo, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi Rukwa, James Makwinya na Mwenyekiti wa Chama cha Soka Rukwa, Ayubu Nyaulingo,  ambao walikuwa wamefungiwa kutokana na kufanya uchaguzi wakati TFF iliwazuia.

 

Katika hatua nyingine, Tarimba amesema kuhusiana na adhabu ya Damas Ndumbaro, imeshindwa kupitiwa kutokana na kutopokea ombi la kuipitia, huku pia akiiomba TFF kuangalia kama kuna barua za watu mbalimbali walioomba kupitiwa kwa adhabu zao wazifikishe kwenye kamati yake ili waweze kuzifanyia kazi.

NA OMARY MDOSE | GLOBAL PUBLISHERS

Leave A Reply