Haji Manara Aipa Somo Yanga SC

OFISA Habari wa Klabu ya Simba, Haji Manara, ameushauri uongozi wa Klabu ya Yanga kujiandaa vizuri kama ni kweli wanataka kuingia katika mabadiliko ya mfumo wa kiuendeshaji wa klabu yao.

 

Hivi karibuni, Yanga walikuja na kampeni iliyopewa jina ‘Twenzetu Kwenye Mabadiliko’ wakiwa na dhamira ya kubadilisha mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo unaosimamiwa na mdhamini wao, Kampuni ya GSM.

 

Akizungumzia hatua hiyo, Manara alisema: “Kwanza napenda kuwapongeza kwa hatua ambayo wanataka kuiendea.

 

“Lakini pia napenda kuwakaribisha huku tulipo kwa kuwa Simba tayari ilishapita hatua hiyo na yote kwa yote napenda kuwaasa watani zangu Yanga wajiandae vya kutosha kwani mchakato huu siyo rahisi na unahitaji weledi wa kutosha ikiwemo kubadilisha mtazamo wa kifikra.

SHANGWE la MASHABIKI baada ya LIGI KUFUNGULIWA – “Yule RAIS Ana BUSARA SANA”


Loading...

Toa comment