The House of Favourite Newspapers

Manara Afunguka Nafasi Yake Kuchukuliwa -Video

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara.

OFISA Habari wa Klabu ya Simba, Haji Manara, leo Agosti 20, 2019, amesema yeye ndiye msemaji wa klabu hiyo kupitia nafasi ya Ofisa Habari.

 

Ameyasema hayo baada ya tetesi kuwa uongozi mpya wa Simba umepata viongozi wapya ikiwemo nafasi ya Ofisa Habari inayochukuliwa na mtangazaji wa Azam TV, Gift Macha.

 

Akizungumzia mechi ambayo Simba itacheza na UD Songo ya Msumbiji katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika Agosti 25, mwishoni mwa wikikatika Uwanja wa Taifa, alisema utaanza saa 10:00 jioni  na viingilio vitakuwa: mzunguko Sh. 5,000, VIP B na C  (15,000), VIP A  (30,000), Platinum (100,000) na Platinum Plus (150,000).

Comments are closed.