The House of Favourite Newspapers

Haji Manara: Yanga ni Klabu Kubwa, Itashinda Kila Taji – Video

0
ALIYEKUWA Msemaji wa Klabu ya Simba, Haji Manara ametambulishwa rasmi kujiunga na Klabu ya Yanga kuwa msemaji wa mabingwa hao wa kihistoria Ligi Kuu Tanzania Bara.
Manara ametambulishwa leo Jumanne, Agosti 24, 2021na uongozi wa Klabu hiyo wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa Serena Hotel jijini Dar es Salaam.
“Namshukuru Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema kwa kutujalia kukutana hapa siku ya leo katika jambo hili ambalo ni kubwa na linaloweza kutuonyesha standards ambazo tunapaswa kwenda nazo katika ufanyaji kazi.
“Nimefanya kazi Simba kwa mika takribani saba sasa kwa kadri nilivyojaliwa, huenda nilifanya vizuri kama na huenda kuna watu wamewachukizwa kwa hiki, lakini katika press yangu nilisema kama binadamu siwezi kuvumilia niliyofanyiwa.
“Wengine watasema leo Simba kesho Yanga, mimi ni professional, kama kocha au mchezaji, anaweza kwenda timu yoyote, mimi ni msemaji, nitangaze rasmi kwamba nimejiunga na klabu kubwa kuliko zote Afrika Mashariki na Kati. Huu ukubwa mnaousema ninao ni lazima nifanye kazi na klabu kubwa, klabu ambayo itanipa nafasi kushirikiana nao.
“Baada press yangu nilipotoka Simba zilikuja ofa nyingi, waliponiambia viongozi wa Yanga kwanza nilishangaa, wakaniambia sisi tunataka tufanye kazi na wewe, lakini baadae nikaona wako siriazi, sikujiuliza mara mbili.
“Mimi napenda vikombe, Yanga wakanieleza namna walivyosajili nafurahi kujiunga na klabu ambayo ninaamini itashinda kila taji msimu ujao.
 

“Siendi Yanga kwa sababu ya jambo lolote, ninaamini Yanga watanipa nafasi ambayo nitaitumikia, kule nilibanwa sana, sina tatizo na Simba, nilisema vizuri kabisa kwamba sijawahi kuwa na tatizo na Simba, walionifanyia nimeshayasema.

 

“Ninachoomba viongozi mnipe sapoti tuijenge Yanga, kama mliniona Simba nikiwa vile, huku nitakuwa mara kumi. Shukrani yangu kwenu ni kufanya kazi kwa asilimia 100, niwahakikishie baada ya Desemba, Yanga itakuwa kila kitu. Mimi ndio nilikuwa nawabeba, sasa hivi wanahangaika tu, hata jambo lao wameshindwa wala sitawacharura.

 

“Mimi nina moyo, ofa ya Yanga angekuwa mtu mwingine angesaini hapo hapo, nimeshauriana na familia yangu, nawashukuru Simba kwa sapoti yenu sasa ni zamu ya kuifanyia kazi Yanga. Mabingwa mara 27.

 

“Yanga ni kubwa mno, sio timu ya kulalamikia TFF wala Bodi ya Ligi, twendeni tukafanye kazi, tutashinda uwanjani, tutengeneze confidence kwa viongozi, wachezaji na mashabiki wetu. Nitafanya kazi kama punda mwenye njaa kuhakikisha Yanga inatimiza malengo yake.

 

“Mtauliza kwamba nilikuwa nawacharura Yanga, hiyo ndiyo soka, niliwatumikia Simba lakini sasa hivi ni zamu ya Yanga, ndio maana nimevaa jezi ya Yanga, mama Yangu na mke wangu wapo hapa. Tamasha la Jumapili njooni uwanjani, nawaambia haijawahi kutokea.

 

“Naongea kama msemaji wa Mabingwa mara 27, kesho saa 5:00 tunakwenda kuzindua jezi kweli, haina makorokoro, jezi ya mpira, jezi ya nyumbani, ya ugenini na kit ya tatu na casual wear pale Mlimani City,” amesema Haji Manara, Msemaji wa Yanga.

Leave A Reply