The House of Favourite Newspapers

Haji Manara: Nitakuwa Rais wa Fifa

0

MKUU wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Haji Sunday Manara, amesema kuwa kama akiamua anaweza kuwa hata Rais wa Shirikisho la Soka la Kimatafa (Fifa).

 

Manara amefunguka kuwa kama ameweza kuhimili kuwa kiongozi wa Simba kwenye nchi ambayo ipo pia na timu ya Yanga na presha za soka la Tanzania, basi hicho ni kipimo tosha kuwa anaweza kuwa Rais wa Fifa bila shida.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Manara alisema anaweza kuwa Rais wa Fifa kwa sababu kule hawana presha na ujanjaujanja, wanazingatia weledi, jambo ambalo yeye analimudu na hata ikitokea kuwa kuna presha halitakuwa jambo geni kwa kuwa ameishi kwenye siasa za Simba na Yanga kwa miaka mingi.

 

“Mimi naweza kuwa hata Rais wa Fifa na nikaongoza vema, unajua kuwa kiongozi wa Simba au Yanga kwa muda mrefu siyo jambo ndogo, kuna presha na siasa za kila aina ambazo lazima uwe ngangari kweli.

 

“Sasa kule Fifa hakuna ujanjaujanja wala presha kama za hapa, kwa hiyo naweza kuliongoza lile shirikisho kwa namna zote, kiweledi hata kisiasa kama za hapa kwetu,” alisema Manara.

STORI: ISSA LIPONDA, Dar es Salaam

Leave A Reply