Hakimu Dar Kortini kwa Tuhuma za Rushwa – Video

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Kinondoni, jana Jumatano, Septemba 11, 2019, iliwafikisha mahakamani watuhumiwa watatu wa rushwa akiwemo Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo jijini Dar es Salaam, baada ya kukamilika kwa uchunguzi dhidi yao.

 

Takukuru imesema watuhumiwa hao ni Omary Mohammed Abdallah (40) aliyekuwa Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Magomeni jijini Dar, ambaye ni mkazi wa Kijitonyama kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa kiasi Tsh 703,000, Joseph Balongo (37) mfanyabiashara na mkazi wa Kibamba kwa kosa la kupokea rushwa ya Tsh 498,000 kinyume na sheria.

 

Imeelezwa kuwa, hakimu huyo alimtaka mtoa taarifa (jina limehifadhiwa na TAKUKURU) ampatie Tsh 1,000,000 ili amsaidie katika kesi ya mirathi iliyokuwa mbele yake. Baada ya Takukuru kufanya uchunguzi na kubaini kuwa ni kweli ilimtia nguvuni.

 

Aidha, Takukuru imemfikisha mahakamani Bw. Nelbert Malevo (33) mkazi wa Wazo, Dar es Salaam, ambaye ni Katibu wa Kamati ya Upimaji Viwanja katika Mtaa wa Nyakasangwe kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa. Inadaiwa kuwa aliomba Tsh milioni 2.5 na akapokea Tsh laki 5 ili ampe kiwanja mtoa taarifa (jina limehifadhiwa na Takukuru).

 

TAZAMA TUKIO HILO HAPA


Loading...

Toa comment