The House of Favourite Newspapers
gunners X

Hakimu Akataa Msokoto wa Bangi Kesi ya Wema

0

Hakimu Mkazi Kisutu

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imekataa kupokea ushahidi wa msokoto wa bangi na vipisi viwili vya madawa hayo ya kulevya katika kesi inayomkabili mwigizaji Wema Sepetu.

Hakimu Mkazi Kisutu
Uamuzi huo umetolewa na Hakimu, Thomas Simba, aliyesema mahakama haiwezi kupokea vielelezo hivyo kwa sababu msokoto wa bangi na vipisi vina kasoro kwa kuwa shahidi hakuvifafanua mahakamani. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 12 mwaka huu.

NA DENIS MTIMA/GPL

Leave A Reply