The House of Favourite Newspapers

Hakuna namna, mtapigwa tu

0

SIMBA YANGA (7)
YANGA na Simba zimeshinda mechi zao za katikati ya wiki hii, lakini nyuma ya ushindi huo makocha wa timu hizo hukumbana na mazingira magumu sana.

Mazingira hayo magumu ndiyo yanayozifanya timu zao kuongeza ujuzi na mbinu zaidi kuweza kufanya vizuri.

Yanga sasa ipo kileleni mwa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 15 ikifuatiwa na Azam FC yenye pointi kama hizo, isipokuwa yenyewe imezidiwa kwenye mabao ya kufunga na kufungwa.

SIMBA YANGA (5)Simba yenyewe ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 12 katika mechi tano, sawa na Yanga na Azam. Kocha wa Yanga, Hans van Der Pluijm, raia wa Uholanzi, timu yake haijafungwa, lakini ameliambia Championi Jumamosi: “Tunashinda kwa tabu sana kwani mambo hubadilika katika kila mechi.

“Huwa hatuna jinsi kwani hulazimika kubadilisha mbinu zetu za ushindi kila mara kulingana na hali tunayokutana nayo uwanjani, tazama Simba walitujazia viungo tukashindwa kupita katikati wakati wa kushambulia.

“Tukacheza pembeni zaidi na tukafanikiwa kushinda (mabao 2-0), mechi na Mtibwa (Sugar) uwanja haukuwa rafiki kwetu, pia wenzetu walikamia kupita kiasi, lakini wakati wa mapumziko nilibadili kitu na tukashinda (mabao 2-0),” alisema Pluijm.

Alisema kutokana na Uwanja wa Jamhuri uliopo Morogoro kutokuwa mzuri sehemu ya kuchezea, hakutaka wachezaji wake wachezee sana mpira, pia aliwataka kutokubali kugongana na wapinzani wao na kweli walifanikiwa.

“Naamini tukiendelea kucheza hivi tutaendelea kufanya vizuri katika mechi zetu zinazofuata,” alisema Pluijm.

SIMBA NAO HIVYOHIVYO

Kocha wa Simba, Dylan Kerr, amesema hata yeye anapata ugumu katika mechi zake lakini huwa hana jinsi zaidi ya kuongeza mbinu za kupata ushindi kwenye mechi zake.

“Kwa muda mfupi niliokuwa Simba, kuna vitu vingi nimejifunza na kubwa ni kupaniwa kupita kiasi na timu pinzani katika kila mechi, sasa mimi kila nikigundua hali hiyo nabadili mbinu na napata ushindi.

“Katika mechi dhidi ya Stand United (Simba ilishinda bao 1-0), tulianza kucheza 4-4-2, mambo yakawa magumu nikawaelekeza kucheza 4-3-3 tukapata bao lakini nina mfumo wa 4-5-1 pia,” alisema Kerr, raia wa Uingereza.

Leave A Reply