Hali ni Mbaya Kitanzi cha R Kelly… Kumbe Alifunga Ndoa na ‘Katoto’?

Image result for r kelly Aaliyah
KUTOKA nchini Marekani, staa wa muziki R Kelly akiwa anaendelea kusota rumande kwa kesi yake ya unyanyasaji wa kingono kwa wasichana wadogo, taarifa mpya zinasema kuwa waendesha mashtaka kwa sasa hawana mpango kumuachia kabisa, na kwamba wamepanga kutumia ndoa yake R Kelly aliyofunga kwa siri na mwanamuziki Aaliyah mwenye umri wa 15 kama uthibitisho.
Image result for r kelly Aaliyah
Mtandao wa Pagesix umeripoti kuwa ndoa ya R kelly aliyofunga kwa siri mwaka 1994 na mwanamuziki ambaye kwa sasa ni marehemu Aaliyah alipokuwa na umri wa miaka 15, ndoa hiyo itatumika kama ushaidi ili kuthibitisha kama kweli R Kelly alikuwa mnyanyasaji wa kingono kwa wasichana wadogo.

Image result for r kelly jail

Mwanamuziki R Kelly bado yupo rumande akiwa katika ulinzi mkali kwenye jela ya peke yake ambapo haruhusiwi kuonana na mtu yoyote na huwa anapata Dk.15 tu za kuongea na simu kwa mwezi na vilevile anaruhusiwa kuoga mara 3 tu kwa wiki.


Loading...

Toa comment