Hali ya Shumi Yadaiwa Kuwa Tete Ughaibuni

Shumileta

 

MWIGIZAJI wa kitambo Bongo, Jennifer Mwaipaja ‘Shumileta’ au ‘Shumi’ anadaiwa kuwa na hali tete ya kimaisha nchini India kufuatia kile kilichotajwa kuachana na bwana’ke aliyekuwa akiishi naye, raia wa Nigeria hivyo kwa sasa anatafuta msaada wa kurejea nyumbani, Tanzania.

 

Akizungumza na Wikienda, mmoja wa marafiki wa karibu na Shumileta ambaye pia ni msanii wa filamu za Kibongo alisema kuwa, alipata taarifa za masaibu hayo ya Shumileta kutoka kwa mmoja wa wanafamilia yake na kwamba wako kwenye mipango ya kumsaidia arejee nyumbani kuendelea na maisha.

 

“Ndugu wako kwenye hatua za mwisho kuhakikisha wanamsaidia kurudi nyumbani,” alisema ‘kikulacho’ huyo.

 

Wikienda liko kwenye msako mkali wa kuwatafuta ndugu wa msanii huyo ili kujiridhisha juu ya madai hayo kuhusu ndugu yao na kila kitu kikikamilika, tutarejea hapa kukujuza kuhusu hali ya Shumi.

 

Stori: Brighton Masalu | IJUMAA WIKIENDA |Dar

 

VIDEO: Mastaa Elizabeth Michael (Lulu) na Joti Walivyotokelezea Kwenye Harusi

Toa comment