Halima Mdee Afanyiwa Upasuaji, Alazwa Aga Khan

Mbunge wa Kawe jijini Dar es salaam kupitia CHADEMA Halima James Mdee, amelazwa katika hospitali ya Aga Khan jijini Dar es salaam akipatiwa matibabu.

 

Taarifa zilizothibitishwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itikadi na uenezi wa CHADEMA, John Mrema amesema kwamba Halima Mdee amefanyiwa upasuaji wa kutolewa uvimbe aliokuwa nao tumboni.

 

“Amefanyiwa upasuaji alikuwa na uvimbe tumboni. ..yuko Agakhan”, amesema John Mrema.

Hii leo baadhi ya Wabunge wametoa ujumbe wao wa pole kumtakia Mbunge huyo kupona kwa haraka, ili aweze kurejea kwenye majukumu yake ya kawaida.

 

“Nilikuja hospitali juzi (Alhamisi) saa tisa alasiri kwa ajili ya kuangalia afya yangu, ila madaktari baada ya vipimo wakabaini tumboni kuna tatizo na kunishauri nifanyiwe upasuaji haraka iwezekanavyo, Nipo vizuri na kati ya kesho au Jumatatu madaktari wataniruhusum,” amesema Mdee.

Loading...

Toa comment