The House of Favourite Newspapers

HALIMA WA MBAGALA AIBUKA KIDEDEA DROO YA MWISHO YA TUSUA MAISHA -VIDEO

Usiilalie bahati ya mwenzako mlango wazi! Hivyo ndivyo unavyoweza kusema kufuatia mwanadada Halima Jabir wa Mbagala ameibuka mshindi wa droo ya 12 na ya mwisho ya Shindano la Tusua Maisha na Global, iliyorushwa mubashara kupitia Global TV Online.

 

Hadija Shaban, mfanyabiashara kutoka Morogoro yeye amejishindia ada ya shule, Hamis Mohamed wa Kinondoni jijini Dar es Salaam aliyejishindia dinner set na Vaileth Mtilega wa Kiwalani aliyejishindia jezi.

 

Ukiwatoa washindi wa pikipiki, ada ya shule, dinner set na jezi waliopatikana jana, washindi 11 waliopata bahati ya kuondoka na pikipiki mpya katika droo za mwanzo ni Richard Tanganyika, mfanyabiashara ndogondogo anayemiliki genge katika eneo la Mdaula, Chalinze mkoani Pwani aliyefungua dimba kwa kushinda pikipiki ya kwanza.

 

Amiri Bakari, mkazi wa Ubungo National Housing, aliibuka mshindi wa pikipiki katika droo ya pili, akafuatia Solomon Mapunda, mkazi wa Majohe jijini Dar es Salaam aliyeng’ara katika droo ya tatu huku Hassan Shekwavi ambaye ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, Railway Quarters iliyopo Kata ya Tambuka mjini Dodoma akiibuka kuwa mshindi wa nne.

 

Wengine ni Emanuel Tenga, mkazi wa Moshi, Kilimanjaro aliyetangazwa kuwa mshindi wa pikipiki katika droo ya tano, Erasto Luponelo, mkazi wa Makambako mkoani Njombe aliyeshinda katika droo ya sita na Said Katambo wa Nachingwea, Lindi aliyeibuka mshindi wa pikipiki mpya katika droo ya saba.

 

Katika droo ya nane, Jackson Bwire, msomaji kutoka Ukerewe, Mwanza aling’ara na kujishindia pikipiki mpya, Simba Ramadhan, mkazi wa Mbezi akaibuka kidedea katika droo ya tisa, Ramadhan Mohamed wa Zanzibar akatusua katika droo ya kumi huku Bolen Kilimba, akishaini katika droo ya 11.

 

“Tunawashukuru sana wasomaji wote walioshiriki, najua kila mmoja alitamani kushinda lakini katika mashindano kuna kupata na kukosa. Nawapongeza wote walioshinda kuanzia droo ya kwanza mpaka mpaka ya mwisho na kwa wale ambao hawakubahatika, wasikate tamaa, tukutane kwenye shindano lingine ambalo tutalitangaza ‘soon’. Nawasihi waendelee kutuunga mkono kwa kusoma magazeti ya Global Publishers ambayo ni Ijumaa Wikienda, Uwazi, Amani, Championi, Risasi, Ijumaa na Spoti Extra kwani yamesheheni mambo mbalimbali. Ahsanteni sana nyote mlioshiriki, tunawapenda sana wasomaji wetu,” alisema Abdallah Mrisho, Meneja wa Global Publishers.

Comments are closed.