The House of Favourite Newspapers

Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Yampitisha Dkt. Samia kuwa Mgombea Pekee wa nafasi ya Mwenyekiti Taifa

0
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM)Taifa Rais Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan akikagua maandalizi mbalimbali ya Mkutano Mkuu wa 10 wa Chama unaotarajiwa kufanyika kuanzia kesho tarehe 07-08 Desemba, 2022 katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.

Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imempitisha Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Mgombea pekee wa nafasi ya Mwenyekiti wa CCM Taifa kwa mwaka 2022 hadi 2027 na jina lake litapelekwa kwenye Mkutano Mku siku ya kesho Desemba 07, 2022 kwa ajili ya kupigiwa kura.

Na kwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti Halmashauri Kuu imempitisha Kinana kuwa Mgombea kwa kiti cha Makamu Mwenyekiti Bara na Dkt. Hussein Mwinyi kwa upande wa Zanzibar

Taarifa hiyo ya Chama imetolewa na Katibu wa Siasa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho Shaka Hamdu Shaka leo Desemba 06, 2022 wakati akitoa taarifa ya kuelekea Mkutano Mkuu wa CCM December 07 na 08 jijini Dodoma.

Leave A Reply