The House of Favourite Newspapers

Halotel, StarTimes waleta kombe la dunia kiganjani  

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Mhina Semwenda Halotel akizungumza na waandishi wa Habari katika uzinduzi wa huduma mpya itakayo wawezesha wateja wa mtandao wa Halotel kuangalia mechi za kombe la dunia kupitia simu zao za kiganjani kwa gharama nafuu . Kulia ni Meneja Masoko wa  Startimes David Malisa. 
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Mhina Semwenda Halotel na Meneja Masoko wa Startimes David Malisa  kwa pamoja wakionesha namna ambavyo  mteja wa Halotel anavyoweza kuangalia mpira kwenye simu yake ya mkononi kupitia App ya Star times.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Mhina, Semwenda Halotel (kulia) na Meneja Masoko  wa  Startimes, David Malisa  wakionyesha ishara ya ushirikiano wa uzinduzi huo wa Halotel na Startimes.

 

 

HUKU mshike mshike wa kombe la dunia ukiendelea kukoleaKampuni ya Mawasiliano ya Simu ya Halotel kwa kushirikiana na Kampuni ya StarTimes wamezindua huduma mpya itakayo wawezesha wateja wa mtandao huo kuangalia mechi za kombe la dunia kupitia simu zao za kiganjani kwa gharama nafuu.

 

Huduma hii itawawezesha wateja wa Halotel na StarTimes kutazama Soka kwenye simu zao kwa gharama nafuu sana, huduma hiyo inawapatia wateja intaneti ya uhakika tena yenye kasi kwa masaa 24 bila kikomo.

 

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Halotel, Mhina Semwenda, amesema huduma hiyo itawawezesha wateja wa Halotel nchini nzima kufurahia kutazama mechi za kombe la dunia kupitia simu za mikononi (Smartphone) kwa urahisi na kwa gharama nafuu kwa kutumia intaneti ya uhakika tena yenye kasi kwa masaa 24 bila kikomo.

 

“Kuanzia sasa wateja wa Halotel wanaweza kupakua Application ya Startimes kupitia simu zao za Android na watalipia kuanzia shilingi 2000 na watapata GB 1 ambayo wanaweza kuitumia kuangalia mechi zote za kombe la dunia kwa intaneti yenye kasi. Alisema Semwenda.

 

“Jinsi ya kufanya malipo mteja wa Halotel anapaswa kufungua Application ya Star times na baada ya hapo atafuata maelekezo ya kununua vifurushi kuanzia vya siku, wiki hadi mwezi mzima,” Alihitimisha Semwenda.

 

Kwa upande wake Meneja Masoko wa StarTimes, David Malisa Alisema, “Ukiwa unatumia intaneti ya Halotel ni rahisi zaidi kulipia na kutumia StarTimes App ambayo ina burudani na mechi zote za Kombe la Dunia. Kwa watumiaji wa mitandao mingine wanalipia maudhui pembeni na intaneti au data pembeni, ukilipia huduma hii unakuwa umelipia maudhui na intaneti kwa pamoja. Pia unaweza kutumia Intaneti hii bila kikomo kwa masaa 24 hata bando inapoisha utaendelea kupata Intaneti ya kutumia kwenye StarTimes App”. Alisema Malisa.

 

Hii ni huduma ya kwanza kabisa Tanzania ambayo itamruhusu mteja kuendelea kupata intanenti hata baada ya bando lake kuwa limekwisha. Ushirikiano baina ya StarTimes na Halotel ni katika hatua ya kusogeza Burudani ya kandanda la kimataifa katika Simu za Mkononi.

Kuhusu Halotel;

Halotel ni chapa ya Viettel Tanzania Ltd, mwanachama wa Viettel Group. Viettel ni kampuni kubwa ya mawasiliano ya simu nchini Vietnam yenye mapato karibu dola bilioni 11 katika mwaka 2015. Mbali na Vietnam, Viettel imewekeza katika sekta ya mawasiliano katika nchi 10 kote 03 mabara, ikiwa ni pamoja na; Cambodia, Laos, Timor Leste, Myanmar kwa Asia Msumbiji, Cameroon, Burundi, Tanzania kwa Afrika na Haiti, Peru ajili ya Amerika. Halotel ilianza rasmi kutoa huduma Oktoba 15, 2015, na huduma za simu katika maduka 30 kote nchini. Halotel nchini Tanzania tayari imepanua huduma za simu kwa mikoa yote  vijijini na mijini.

 

Kuhusu StarTimes

 

StarTimes ni kampuni ya Matangazo ya kidigitali inayoongoza Africa, ikihudumia zaidi ya wateja milioni 10 katika bara zima. StarTimes inamiliki jukwaa la maudhui lenye chaneli 480 zikiwemo chaneli za Habari, filamu, tamthiliya, michezo, burudani, vipindi vya watoto, mitindo, dini na vingine vingi. Matazamio ya Kampuni ni “Kuhakikisha kila familia ya kiafrika inapata, inamudu, inatazama na kushiriki kwenye Uzuri wa Televisheni ya kidigitali”

Comments are closed.