The House of Favourite Newspapers

Halotel Yashinda Tuzo za Chaguo la Mteja Afrika 2023 kwa Mwaka wa Nne Mfululizo

0

Halotel, Kampuni ya Mawasiliano nchini Tanzania yenye mtandao ulioenea nchini, kwa heshima kubwa imetunukiwa tuzo ya “Mtandao Bora unaotoa Huduma za Mawasiliano kwa Bei Nafuu Zaidi na Rafiki kwa Mteja Mwaka 2023” katika tuzo za Chaguo la Mteja Afrika. Ambazo zilizotolewa mbele ya Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Dotto Biteko.Hii ni kwa mwaka wa nne mfululizo, kuanzia 2020 hadi 2023, ambapo Halotel imeshinda tuzo hii ya heshima katika kipengele hicho hicho.

Tuzo za Chaguo la Mteja Afrika, zilizoanzishwa kwa lengo la kukuza ubora wa biashara mbalimbali kupitia chaguo la Mteja, ambapo Tuzo hizi zinajumuisha kipengele cha Makampuni yanayotoa huduma za Mawasiliano nchini, pamoja na vipengele vingine. Halotel ilikabiliana na ushindani mkali katika kipengele cha watoa Huduma za Mawasiliano, lakini azma yake ya kuhakikisha inatoa huduma nafuu na zinazokidhi mahitaji ya wateja ilileta utofauti wa kipekee.

Mkurugenzi wa Biashara wa Halotel, Bw. Abdallah Salum, alitoa shukrani zake kwa wateja kwa imani yao na kuendelea kuunga mkono kwa kutumia huduma za Halotel. Alisema, “Tunajisikia heshima kubwa kwa kupokea Tuzo za Chaguo la Mteja Afrika kwa mwaka wa nne mfululizo. Hii ni matokeo ya moja kwa moja ya imani ambayo wateja wetu wanatupa na kura walizotupigia. Tunawashukuru kwa imani yao endelevu na tunaahidi kuboresha viwango vya juu katika kutoa huduma za mawasiliano ya simu.”

Tunawashukuru pia waandaaji wa Tuzo hizi za Chaguo la Mteja Afrika, kwa kuandaa tuzo hizi na kuwapa wateja wetu fursa ya kutoa maoni yao kupitia kupiga kura hii inakuza ushindani na kuhakikisha tunatoa huduma bora zenye kukidhi mahitaji ya wateja wetu wote. Ushindi huu ni ushuhuda wa dhamira ya Halotel ya kuendelea kutoa huduma bora na yenye viwango vya juu kwa wateja. Wakati sekta ya Mawasiliano inavyoendelea kubadilika, Halotel inaendelea kutoa suluhisho za ubunifu na nafuu za huduma zinazokidhi mahitaji mbalimbali ya wateja wake.

Bw. Salum pia alisisitiza kuwa Halotel itaendelea kuzingatia kutoa huduma bora, kuhakikisha kuwa mahitaji ya kila mteja yanazingatiwa na kukidhiwa. “Halotel imejitolea kuwa ‘Pamoja kwa Ubora,’ na tutazidi kushirikiana katika juhudi zetu za kuimarisha uunganisho, upatikanaji wa huduma kwa gharama nafuu, na uzoefu wa huduma bora kwa wateja,” aliongeza.

Halotel inatoa shukrani zake za dhati kwa Consumer Choice Awards Africa kwa kutambua mchango wake katika Sekta ya Mawasiliano. Kampuni inatarajia kuendelea na safari yake ya Kuhakikisha watanzania na wateja kwa ujumla wananufaika na Mtandao huu wa Mawasiliano katika kukidhi mahitaji yao mbalimbali katika Nyanja zote ikiwemo kiuchumi, na kijamii maana inaamini iko pamoja katika kutoa ubora na uvumbuzi,wa huduma muhimu kwa wateja wake.

Leave A Reply