The House of Favourite Newspapers

Halotel Yatoa Tabasamu Kwa Yatima Kuelekea Sikukuu ya Eid El Fitr

0
Mkurugenzi wa Halotel mkoa wa Pwani Bw. Rodrick Paul (kushoto), pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Masoko Halotel Sakina Makabu (kati) wakimkabidhi Mkurugenzi wa Kituo cha Fadhillah Orphanage Centre  Bi Sureya Shehe (kulia) mbuzi wawili pamoja na msaada wa  vitu na mahitaji mengine maalum ikiwemo vyakula kama mchele, unga, mafuta ya kupikia, na vinginevyo leo kama mkono wa kusherehekea Sikukuu ya Eid ul Fitr inayotarajiwa hivi karibuni ikiwa ni moja ya program ya kurudisha kwa jamii kwakusambaza upendo na tabasamu kwa watoto yatima wa kituo hicho kilichopo eneo la Misugusugu Mkoani Pwani.

Katika kuelekea Sikukuu za Eid ul Fitr, Kampuni ya simu za mkononi ya Halotel Tanzania imetoa msaada kwa kituo cha watoto yatima mkoa wa Pwani kama moja ya program ya kurudisha kwa jamii katika kuboresha, kuonesha upendo na kuwaletea tabasamu watu wanaoishi katika hali ngumu, kupitia utekelezaji wa majukumu ya Jamii ya watanzania.

Kampuni hiyo imetoa msaada wa vyakula, mbuzi, na mahitaji mengine ya muhimu ya kijamii kwa kituo cha Watoto Yatima kiitwacho “Fadhillah Orphanage Centre”, kilichopo eneo la Misugusugu katika mkoa wa Pwani ikiwa ni mkono wa Siku Kuu ya Eid ul Fitr.

Wakikabidhi msaada huo, Mkuu wa Kitengo cha Masoko Halotel, Sakina Makabu alisema msaada huo ni utaratibu wa kawaida wa kampuni hiyo kuikumbuka jamii hasa watotowaliopo katika mazingira magumu.

Aidha mbali na kampuni hiyo kutoa msaada huo kwa Watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu, wamezielekeza ofisi zao mikoa mbalimbali Tanzania kusaidia makundi hayo kama walivyofanya Pwani. Alisema Sakina.

Baadhi ya wafanyakazi kutoka katika Kampuni ya Mawasiliano Halotel, baadhi ya watoto na Mkurugenzi wa kituo cha Fadhillah wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa makabidhiano ya msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo vyakula kwa kituo cha watoto yatima cha Fadhillah Orphanage Centre kilichopo eneo la Misugusugu mkoani Pwani kwaajili yakusherekea Sikukuu ya   Eid ul Fitr inayotarajiwa hivi karibuni ikiwa ni moja ya program ya kurudisha kwa jamii kwakusambaza upendo na tabasamu kwa watoto yatima wa kituo hicho.

Kituo hiki cha Fadhillah, kitakachopokea msaada huo kinalea na kusomesha watoto 168 ambao wote ni yatima kwa kuwapoteza wazazi wao au nyinginezo. Watoto wengi kati yao walipitia changamoto nyingi, na kituo hiki kinatoa mazingira salama na ya upendo ambapo wanaweza kupata huduma na msaada wanaohitaji.

“Leo tunatoa mifuko ya kilo 150 ya mchele, kilo 50 za maharage, ndoo za lita 80 za mafuta ya kupikia, kilo 100 za unga wa mahindi, kilo 50 za sukari, Tambi mifuko 100, mbuzi wawili (2), sabuni za usafi wa mwili na za kufulia, pampas kwa mtoto asiyejiweza na Watoto wachanga, Pamoja na vifaa kwaajili ya shule. Zawadi hizi lengo lake kubwa ni kutoa tabasamu na upendo kwa watoto hawa katika sikukuu hizi za Eid Mubarak ili na wao waweze kusherehekea na kufurahia kama watu wengine. Aliongeza Sakina

Akizungumza kuhusu msaada huo, Mkurugenzi wa kituo Bi.Sureya Shehe alitoa shukrani zake kwa Halotel akisema, “Tunashukuru sana kwa mchango huu mkubwa kutoka Halotel. Utaleta tofauti kubwa kwa watoto hapa, ambao wanahitaji sana mahitaji ya msingi kama chakula na vifaa vya shule, na zaidi hasa kwa upendo huu kuwawezesha Watoto hawa kufurahia Sikukuu hii ya Eid ul Fitr. Tunathamini jitihada hizi za Halotel kusaidia jamii yetu ya watanzania na tunatarajia waendelee kufanya hivi ili kuboresha maisha ya watanzania.

Mkuu wa Kitengo cha Masoko Halotel Sakina Makabu, akiongea na waandishi wa Habari leo wakati wa makabidhiano ya msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo vyakula kwa kituo cha watoto yatima cha Fadhillah Orphanage Centre kilichopo eneo la Misugusugu mkoani Pwani kwaajili yakusherekea Sikukuu ya Eid ul Fitr inayotarajiwa hivi karibuni ikiwa ni moja ya program ya kurudisha kwa jamii kwakusambaza upendo na tabasamu kwa watoto yatima wa kituo hicho.

Msaada wa Halotel kwa kituo hiki ni moja ya utaratibu ambao utaendelea kutekelezwa mara kwa mara ili kujenga mahusiano mazuri na jamii ambayo pia ni wateja na watanzania kwa ujumla. Utaratibu huo, unatekelezwa kufuatia sera bora ya kampuni hiyo kupitia program za kurudisha kwa jamii mbali na kutoa huduma bora za mawasiliano nchi nzima.

Leave A Reply