The House of Favourite Newspapers

Mpinzani Niger Afungwa Kwa Kuuza Watoto

Hama Amadou akiwa kwenye harakati zake za Kisiasa nchini Niger

Hama Amadou akizungumza jambo kwenye harakati zake za kisias

Kiongozi wa upinzani nchini Niger Hama Amadou amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kupatikana na hatia ya kujihusisha na biashara haramu ya kuuza watoto wachanga kwa matajiri waliokuwa wanahitaji watoto hao.

Kiongozi huyo ambaye alishika nafasi ya pili kwenye uchaguzi uliofanyika mwaka jana alikuwa anajihusisha na biashara ya kununua watoto kutoka nchi jirani ya Nigeria.

Wakati hukumu hiyo ikitolewa, Amadou na mawakili wake hawakuwepo mahakamani na kila mara alikuwa akikanusha tuhuma hizo na kuzielezea kuwa ni za kisiasa.

Na Mwandishi wetu/GPL

Comments are closed.