The House of Favourite Newspapers

Hamisa: Mimi, Mimba Tena? Si Ingetoka!

Hamisa Mobeto

MWANAMITINDO maarufu na mzazi mwenziye mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’, Hamisa Mobeto amefunguka kuwa hana ujauzito kama watu wanavyoeneza uvumi huo kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.

 

Akizungumza na Amani, wakati akitoa msaada kwenye kituo cha watoto yatima cha CHAKUWAMA, kilichopo Sinza-Mori jijini Dar, Mobeto alisema haiwezekani akawa mjamzito kwa kipindi hiki sababu kwanza mtoto wake bado ni mdogo na maneno mengi ya kejeli yanatolewa dhidi yake mtandaoni.

 

“Watu naona wanachukulia kubeba mimba ni kitu rahisi sana lakini wangetambua mimi nina mtoto mdogo sana lakini kitu kingine waangalie kuwa hata kama ningeshika ujauzito lazima ungetoka maana kila kukicha ni kusimangwa ila muda wangu sahihi ukifika wa kuzaa mtoto mwingine nitafanya hivyo tu,” alisema Mobeto.

Stori: Imelda Mtema, Amani

Comments are closed.