Hamisa Mobeto amepoteza mwelekeo wa maisha!

MWISHONI mwa wiki iliyopita, mwanadada Hamisa Mo­beto kwa mara nyingine ali-make headline kwenye mitandao ya kijamii, baada ya kuanza kuvujishwa kwa taarifa zake za ndani na mmoja kati ya wasiri wake.

 

Kwa wapekuzi wa mitandao ya kijamii, wa­takuwa wanaelewa namaan­isha nini lakini kwa kifupi ni kwamba taarifa zilizokuwa zinavujishwa mitandaoni, zimefunua upande wa pili wa maisha ya msanii na mwanamitindo huyu, ambao pengine wengi walikuwa hawaujui.

 

Naelewa kwamba wakati mwingine mtu asiyeku­penda anaweza kuamua kutumia mitandao ya kijamii kukuchafua na kukufanya uonekane si lolote si cho­chote mbele ya jamii! Najua pia kwamba wapo baadhi ya watu ambao ni mahodari wa kutengeneza habari za uongo kuhusu watu fulani kwa sababu wanazozijua wao wenyewe.

 

Lakini pia Waswahili wanasema lisemwalo lipo, kama halipo basi laja! Yamezungumzwa mambo mengi kuhusu Hamisa lakini kubwa nataka nizungumze na mwanadada huyu kuhusu suala la uhusiano wake wa kimapenzi na picha anayoijenga kwenye jamii.

Hamisa amepoteza utu­livu katika mapenzi, kila ku­kicha anaibuka na skendo mpya kuhusu mapenzi, leo ukisikia hili basi ujue kesho linakuja zito zaidi ya lile la jana. Nakukumbusha kwamba Hamisa ni mama wa watoto wawili.

 

Wa kwanza ni yule aliyezaa na bosi mmoja wa redio maarufu Bongo, walikuwa kwenye uhusiano ‘siriasi’ na pengine wengi walianza kumjua Hamisa Mobeto kipindi hiki.

Baadaye sijui ikawaje, penzi hilo likafa lakini mara zikaanza kuibuka tetesi kwamba anatoka kimapen­zi na Diamond Platnumz, kila mtu akawa anakanu­sha lakini mwisho wa siku, uhusiano huo umesababi­sha kupatikana na mtoto mwingine.

 

Kwa hiyo unapomzun­gumzia Hamisa, elewa kwamba unamzungumzia mama wa watoto wawili! Hakuna namna yeyote mama wa watoto wawili anaweza kuwa bado haja­komaa kiakili, Hamisa hana utoto wowote wa kujificha anapofanya haya madudu yake.

Hebu turudi kwenye pointi, katika chating zinazosambaa, inaonesha kwamba kumbe ile safari ya mwanadada Hamisa Mobeto kwenda nchini Marekani, haikuwa ya kikazi kama mwenyewe alivyotaka kuwaaminisha Wabongo.

 

Ilikuwa ni safari ya mapenzi, ambayo ilirati­biwa kwa sura ya kufanya ionekane kwamba mwim­baji huyo wa Madam Hero anakwenda kutan­gaza kazi zake kimataifa, kumbe wapi!

Mwanaume anayeta­mbulishwa kwa jina la Mr Champagne, msanii wa muziki kutoka Jam­huri ya Kidemokrasia ya Congo ndiye anayetajwa kuwa nyuma ya mchongo mzima.

 

Achana na madudu mengine kibao yanayo­tajwa kufanyika katika ziara hiyo ya Hamisa, wiki chache zilizopita ni Hamisa huyuhuyu aliingia kwenye skendo nyingine ya kudaiwa kukwapua mwanaume wa mwana­dada mwingine aitwaye Tahiya.

 

Skendo ikawa kubwa kwelikweli na kusambaa kila kona, huku Hamisa naye akishupaza shingo mithili ya anayesema ‘kwani tatizo liko wapi?’ Mambo anayoyafanya Hamisa, hayafanani kufanywa na mama wa watoto wawili!

 

Inaonesha kuna kitu hakipo sawa kwenye kichwa cha Mobeto, pengine aliyoyapitia yam­emuathiri kisaikolojia kia­si cha kumfanya asielewe tena nini anataka kwenye maisha yake. Anahitaji kusaidiwa huyu. Haya ni maneno dawa ambayo akijitafakari na kuyafanyia kazi, yanaweza kumfaa.

Toa comment