The House of Favourite Newspapers

Hamisa Mobeto na Wema Kimeumana! Baada ya Kupambanisha na Mashabiki

0
Mwanamitindo na msanii wa Bongo Fleva, Hamisa Mobeto ‘Misa’.

 

Mobeto na Wema kimeumana! Ndivyo wanavyosema wafuatiliaji wa habari za wasanii mitandaoni.

Na hii ni baada ya wafuasi wa mwanamitindo na msanii wa Bongo Fleva, Hamisa Mobeto ‘Misa’ kulumbana juu ya jambo lililokuwa likiendelea kati yake na mwanadada Wema Isack Sepetu ‘Wema’.

Inakumbushwa kuwa kipindi kile ambacho Wema aliweza kufikisha wafuasi 10 milioni kwenye mtandao wa Instagram, watu walianza kumpambanisha na Hamisa Mobeto baada ya Wema kuandika mtandaoni kwamba hataki kushindanishwa na msanii yeyote wa kike Bongo.

“Nabaki kuwa wa kike wa kwanza Tanzania kufikisha followers 10 M, basi naombeni kuanzia sasa, msinishindanishe na mtu jamani. Atakaefuata na kunizidi isiwe battle basi wapenzi wangu. Tumefikisha 10M bila nguvu yoyote, nitumie tu nafasi hii kusema ASANTENI na NAWAPENDA,”aliandika Wema insta.

Mwanadada Wema Isack Sepetu ‘Wema’.

 

Hata hivyo baada ya kuposti maneno hayo Wema alikiona cha mtema kuni kwani ‘Timu Hamisa’ ilimjia juu kwa kuandika mengi.

“Wema wa ajabu sana; wenzake wanaringia kununua ma- Range Rover; yeye anafurahia kufikisha wafuasi milioni 10 mtandaoni. Kweli maisha yanabadilika sana,” alisema mmoja wa wafuasi wa Hamisa Mobeto.

 

Baada ya mwanamitindo Hamisa naye kufikisha wafuasi milioni 10 kwenye mtandao wa instagram, kumezua mtafaruku na malumbano kati ya wafuasi wake na wale wa Wema ambao kila upande unaponda upande mwingine.

 

HAMISA AZUNGUMZA

IJUMAA ilimtafuta Hamisa Mobeto na kumuuliza kuhusu yeye kufikisha wafuasi 10 milioni na jinsi wafuasi wake wnavyomponda Wema.

 

Mwanamitindo huyo alisema kwamba kwa sasa yeye yupo ‘bize’ na maisha, hivyo mambo ya mitandao hajihusishi sana.

“Kama wfuasi wetu wanalumbana sijui kwani siku hizi situmiagi muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii. Maisha yangu kwa sasa yananiweka bize kuliko kitu chochote,” alisema Hamisa.

 

STORI: KHADIJA BAKARI

WOLPER AJIBU KWA NINI AMEONEKANA MNYONGE KANISANI; “MIMI NAHESHIMU IBADA, SIWEZI KUWA FREE KIHIVYO”

Leave A Reply