Hamorapa Amzawadia Tisheti Ali Kiba, Adai Ndiye Msanii Anayeongoza kwa Sasa Bongo

MSANII wa Hip Hop anayefanya vizuri kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii Bongo Athuman Omary ‘Harmorapa’ ameibuka na mapya leo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere baada ya kutinga uwanjani hapo kumpokea Ali Kiba sambamba na kumzawadia tisheti iliyoandikwa ‘Kiba Addict’.

Harmorapa

Hamo ameushangaza umma kwa mapenzi yake kwa Ali Kiba kwani inadaiwa alikuwa lokesheni akishuti wimbo wake mpya anaotarajia kuutoa mwezi ujao. Hamorapa aliiacha kazi yake ya kuandaa kichupa chake kipya kutinga fasta uwanjani hapo kumpokea Ali Kiba.

‘Ali kiba ndiye msanii mkubwa kwa sasa Tanzania, namkubali kupita maelezo yaani namkubali kutoka ndani ya damu,’ alisema Hamorapa

Na Salum Milongo/GPL

TAZAMA MAPOKEZI YA ALI KIBA, HARMORAPA ALIVYOMZAWADIA TISHETI
Toa comment