Hamorapa Anaswa Akinunua Kanzu Ya Idd

Harmorapa ambaye ni msanii wa Bongo Fleva, amebambwa katika soko la  Kariakoo jijini Dar kwenye  duka moja maarufu la kuuza kanzu linaloitwa Kanzu Empire, akijinunulia kanzu kwa ajili  ya Sikukuu ya Idd inayotarajiwa kuwa Jumapili au Jumataju ijayo.

Akizungumza na mtandao wa Global Publishers, Hamorapa sliyeongozana na  bosi wake, Irene Sabuka alisema  ameona ajipongeze kwa kujinunulia kanzu nzuri baada ya kufanikiwa kufunga mwezi mzima wa  Ramadhan bila kupumzika. Jina lake halisi msanii huyu asiyeishiwa kiki ni Athuman Omary.

“ Yaani nimekuja dukani hapa  kujipongeza kwa kujinunulia kanzu nzuri  kwa sababu niliweza kufunga mwezi mzima hivyo nikaona natakiwa kwenda msikitini nikiwa nimependeza” alisema Hamorapa.

Toa comment